Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sana na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akipokelewa na
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja
alipofanya Ziara katik ofisi za Baraza hilo leo jijini Dar es
Salaam.Kutoka kulia ni mjumbe wa BMT Bibi. Jenifer Mmasi Shang’a na
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Alex Nkenyenge.
Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sana na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura aakizungumza na
wafanyakazi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) alipofanya Ziara katika
ofisi za Baraza hilo leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sana na Michezo Bibi. Nuru Halfani Mrisho Milao
akizungumza jambo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe.
Annastazia James Wambura (katika) katika ofisi za Baraza la Taifa la
Michezo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa BMT Mohamed
Kiganja.
Katibu Mkuu wa BMT Mohamed
Kiganja akifafanua jambo mbele ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (kushoto) alipofanya
ziara katika ofisi za Baraza hilo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni
Afisa Utumishi wa BMT Bw. Jacob Nduye na wapili kulia ni mjumbe wa BMT
Bibi. Jenifer Mmasi Shang’a.
Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sana na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura, Naibu Katibu
Mkuu na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Alex Nkenyenge
wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja wakati wa
ziara yake katika ofisi za Baraza hilo lep jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sana na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akiwa katika
picha ya pamoja na wafanyakazi wa BMT leo jijini Dar.Kutoka kushoto
waliokaa ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo na wa mwisho kulia
waliokaa ni Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed
Kiganja.
Picha na: Frank Shija, WHUSM
………………………………………………………………………………………..
Na: Frank Shija, WHUSM
BMT yaagizwa kuongeza kasi ya
ufuatiliaji wa viwanja vya michezo vilivyovamiwa nakuvirejesha kwa jamii
kwa ajili ya matumizi ya michezo.
Agizo hilo limetolewa leo na na
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nuru Khalifani
Milao alipofanya ziara katika ofisi za Baraza hilo kwa ajili ya kujionea
hali ya utendaji katika baraza hilo.
Mhe. Wambura alisema kuwa
kumekuwa na changamoto ya maeneo mengi yaliyotengwa kwa shughuli za
kijamii ikiwemo michezo kuvamiwa na watu na kufanya shughuli kinyume na
taratibu.
“Kama ilivyo katika Ilani ya
uchaguzi BMT mnawajibika kufuatilia maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili
ya shughuli za michezo fuatilieni kwa karibu kikiwemo na kile cha
Tandika ambacho tulikwisha anza nacho” Alisema Naibu Waziri.
Aidha Wambura alihimiza Bmt
kuhakikisha inahamasisha ushiriki wa wanawake katika michezo kwa kuwa
michezo ipo kwa ajili ya wote na kuongeza kuwa mbali na mashindano
michezo pia utumika kujenga afya za mwanadamu.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja alisema kuwa pamoja na
changamoto zilizopo watahakikisha wanapiga hatua katika kukuza sekta ya
michezo kwani BMT ndiyo mkono pekee wenye dhamana ya kusimamia michezo
kisheria.
Ata hivyo alielezea changamoto
zinazowakabili katika kutekeleza majukumu yao kuwa ni kuwa ni ufinyu wa
bajeti, upungufu wa wafanyakazi na muingiliano wa Wizara mbili katika
utekelezaji katika ngazi ya Manispaa na Halmashauri Maafisa Michezo
wanawajibika chini ya Wizara ya TAMISEMI hivyo kuna haja ya kukaa pamoja
na kuangalia namna bora ya kushirikiana
No comments:
Post a Comment