Ufinyu wa Bajeti katika sekta ya
michezo umechangia kwa kiasi kikubwa kwa kituo cha Michezo cha kanda ya
Kusini- Songea kushindwa kuendesha mafunzo ya muda mfupi kwa makocha,
marefarii, madaktari wa michezo, uongozi na utawala katika michezo.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa
kituo hicho Eliufoo Nyambi wakati akisoma taarifa ya kituo kwa Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura
wakati alipotembelea kituo hicho ili kuona shughuli za michezo
wanazozifanya.
Nyambi alisema miaka ya nyuma
kituo hicho kimekuwa kikitoa mafunzo ya muda mfupi ya aina tofauti ya
michezo na kufanikiwa kupata wataalamu wa ngazi za makocha, marefa,
madaktari wa michezo, utawala na uongozi wanaotoa mafunzo na huduma za
kimichezo kutoka mikoa 13 na wengine kupata sifa za kujiunga na chuo
cha Maendeleo ya michezo kilichopo Malya wilayani Kwimba.
“Kuanzia mwaka 2011 hadi sasa
kituo hiki hakijatoa mafunzo ya michezo katika mikoa inayoihudumia ya
kanda ya Kusini ikiwa ni pamoja na upimaji wa viwanja hii ni kutokana
na ufinyu wa bajeti uliopo”, alisema Nyambi.
Kwa upande wake Mhe. Naibu Waziri
Wambura alisema nia ya Serikali ni kuimarisha michezo ili watu wapate
muda wa kucheza kwani michezo ni afya, chanzo cha ajira, kujenga
mahusiano mazuri katika jamii na Serikali kupata chanzo cha kukusanya
maduhuli.
Mhe. Wambura alisema Serikali
itaangalia namna ya kukiwezesha na kukiboresha kituo hicho ili kiendelee
kutoa mafunzo hayo ambayo yakifanyika yatasaidia kupunguza gharama
kwakuwa yanawakusanya wanamichezo wengi katika eneo moja na walimu wa
michezo wanaenda kutoa mafunzo.
Naye Kaimu Mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma Mhe. Benson Mpesya ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Songea alisema
hivi sasa mafunzo ya michezo yanatolewa na Asasi binafsi lakini kama
Kituo hicho kitatoa mafunzo itawasaidia washiriki kupata elimu ya
michezo na vyeti vya ushiriki vinavyotolewa na Serikali.
Mwaka 1980 Serikali ilianzisha
vituo vya michezo viwili ambavyo ni kituo cha michezo cha Kanda ya
Kaskazini kilichopo mkoani Arusha na Songea.
Kituo cha Michezo Songea
kinahudumia mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara,
Iringa , Mbeya, Njombe, Ruvuma, Rukwa, Katavi, Dodoma na Songwe |
April 14, 2016
UFINYU WA BAJETI KATIKA SEKTA YA MICHEZO UMECHANGIA KITUO CHA MICHEZO SONGEA KUSHINDWA KUENDESHA MAFUNZO KWA WANAMICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment