Aliyekuwa bondia wa kwanza maarufu
mwenye asili ya Kiafrika, Mohammed Ali, wa Marekani amefariki leo
asubuhi akiwa na umri wa miaka 74.
Kulingana na msemaji wa familia
yake, bingwa huyo wa zamani wa uzani wa juu, anayejulikana sana kote
duniani kwa sababu ya machachari yake katika ngumi, alifariki katika
jiji la Phoenix Arizona, baada ya kulazwa hospitalini Alhamisi.
Alikuwa
na matatizo ya kupumua, hali ambayo ilitatanishwa zaidi na maradhi ya
Parkinson, ambayo ni hali ya mgonjwa kutetemekatetemeaka.
Taarifa ya familia yake imesema kuwa ibada ya mazishi itafanywa nyumbani kwake Lousville, Kentucky.
Alipozaliwa alipewa jina la Cassius Marcellus Clay.
Alipata umaarufu mkubwa aliposhinda medali ya
dhahabu katika mashindano ya Olimpiki yaliyofanyiwa Roma mwaka 1960
katika uzani wa uzito wa kadri au light-heavyweight.
Alipewa jina
la Utani "The Greatest" na alimtandika makonde Mmarekani mwenzake Sonny
Liston mwaka wa 1964 na kushinda taji lake la kwanza la Dunia.
Alikuwa bondia wa kwanza kushinda taji la Heavyweight mara tatu.
Alistaafu mwaka 1981 baada ya kushinda mashindano 56 kati ya 61 aliyoshiriki.
No comments:
Post a Comment