SIKU
moja tu baada ya kuhojiwa na Polisi kwa saa tatu visiwani hapa, Katibu
Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema njia pekee ya kumwondoa
Rais Dk. Ali Mohamed Shein madarakani, ni kuendeleza mgomo baridi.
Maalim
Seif alisema hayo jana alipozungumza na wafuasi wa chama hicho,
Kilimahewa Wilaya ya Mjini Unguja, katika ziara zake za kuimarisha CUF
katika kila wilaya za Zanzibar.
Naibu
Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Salum Msangi, aliwaambia waandishi wa
habari juzi kuwa jeshi lake lilimhoji Maalim Seif kwa saa tatu.
Ingawa
Msangi hakusema walimhoji katika masuala gani, Wakili wa Maalim Seif,
Awadh Ali Said, alisema juzi kuwa mteja wake aliwekwa kati na maafisa 12
wa polisi, ambao walitaka kujua pamoja na mambo mengine, ni kwa nini
hawakatazi wafuasi wake kumwita Rais.
Akizungumza
jana, Maalim Seif alisema mataifa ya nje hayawezi kumwondoa Dk. Shein
madarani lakini kama wananchi na wafuasi wa CUF wataungana kufanya mgomo
baridi, haitafika miezi mitatu kabla hajaachia madarakara.
“Wala msidhani kwamba atakuja Mmarekani kumwondoa Dk. Sheni," alisema Maalim Seif na kuongeza kuwa: "Hii ni nchi, taifa lingine haliwezi kuingilia."
Katibu mkuu huyo alisema anachoweza kufanya Mmarekani ni kuzuia misaada na wameshalianza hilo.
"Sasa
hawa wezetu mataifa ya nje wanatubeba na anayebebwa hujikaza. Tukikaza
uzi huyu bwana miezi mitatu hafiki kwa sababu hana fedha, ataweza vipi
kuiongoza Serikali wakati baadhi ya mataifa yameshazuia misaada yao?" alihoji.
CUF
imegoma kuitambua serikali ya Dk. Shein kwa madai kuwa uchaguzi mkuu wa
marudio wa Machi 20, mwaka huu, uliomwingiza madarakani ni batili.
CUF
inadai kutambuliwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka
jana, ambao ilielekea kushinda na ambao matokeo yake yalifutwa na
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanizbar (ZEC), Jecha Salum Jecha, kwa
madai ya kuwapo kwa kasoro nyingi.
ZEC
ilifuta matokeo hayo licha ya waangalizi wa ndani na wa kimataifa,
wakiwemo kutoka Jumuiya ya Madola, Jumuiya ya Ulaya (EU) na Marekani
kuutangaza kuwa huru na haki.
Akizungumza
katika kikao hicho jana, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazrui,
alisema Maalim Seif ndiye mkombozi wa Wazanzibari kama alivyokuwa
Nelson Mandela wa Afrika Kusini.
Alisema
wana imani kuwa Maalim Seif ndiye Rais wa Zanzibar na wataendelea
kumwita Rais na hakuna wa kuwazuia kwa sababu yeye ndiye aliyeshinda
katika uchaguzi wa Oktoba 25.
Alisema
kitendo cha wafuasi wa CUF kuwatenga wafuasi wa CCM na viongozi wa
Serikali walioko madarakani ni halali na kuwataka wafuasi hao kuendelea
na mgomo huo.
“Hakuna cha kuogopa, endeleeni kuwagomea," alisema Mazrui na kuwataka wasiende katika shughuli zao, mazishi na wanaouza maduka wasiwauzie bidhaa mpaka haki yao irejee.
|
June 2, 2016
MAALIM SEIF AITISHA MGOMO BARIDI UNGUJA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment