KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

June 2, 2016

UNESCO YATAJA CHANGAMOTO ZINAZOKABILI MAENEO YENYE URITHI AFRIKA

LIW5
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni limetaja baadhi ya changamoto zinazoyakabili maeneo yenye Urithi wa dunia barani Afrika hivi sasa
 
Akizungumza  katika Mkutano wa Siku nne  unaofanyika Arusha, Tanzania Mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa  cha Urithi wa dunia kutoka Makao Makuu ya UNESCO Dkt  Mechtild Rossier amesema maeneo hayo mengi barani afrika  yanakabiliwa na changamoto nyingi kutokana na shughuli mbalimbali zikiwemo za binadamu
 
Dkt Rossier amezitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa  ni mabadiliko ya tabia nchi ambapo 16 kati ya 48 yenye  urithi wa dunia  yaliyopo barani afrika  hususani kusini mwa jangwa na sahara  yapo hatarini kutoweka .
 
 
Changamoto nyingine ni kuwepo na migogoro ya vita katika baadhi ya nchi katika bara la afrika, vitendo vya ugaidi, uwindaji haramu, kupanuka kwa  ujenzi wa makazi na kusikosimamiwa vizuri
 
Pia kutokuwepo na kukosekana kwa mipango mizuri na ujenzi holela wa makazi pamoja na uchimbaji w amadini na  mafuta katika maeneo yenye urithi wa dunia.
 
Amyataka mataifa ya bara la afrika kuhakikisha  kwamba yanatoa elimu ya kutosha kwa wananchi wake  juu ya umuhimu wa maeneo hayo kwa faida ya vizazi vijaavyo na dunia
 
Maeneo hayo ni pamoja na  hifadhi ya Taifa ya Serengeti,,Bonde  la hifadhi ya Ngorongoro,Pori la akiba  la Selous,Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro,,Mji Mkongwe wa Zanzibar,,Magofu ya Kilwa kisiwani,na Songo Mnara pamoja na  Michoro ya  Miambani  iliyopo Kondoa Mkoani Dodoma

No comments:

Post a Comment