Katibu tawala mkoa wa
Arusha,Richard Kwitega, amesema kwenye maadhimisho hayo ambayo kilele
chake kitakuwa ni Juni 5 mwaka huu mkoa utapanda miti kwenye maeneo yote
ya mkoa huo lengo ni kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
Amesema shirika la umoja wa
mataifa la mazingira UNEP, limepanga juni 5 kila mwaka ni siku ya
maadhimisho ya mazingira duniani,ili watu wajue umuhimu wa kutunza na
kusimamia mazingira yao.
Kwitega,alisema mwaka huu 2016
maadhimisho ya mazingira kimataifa yanaadhimishwa nchini Angola,yakiwa
na kauli mbiu isemayo uvumilivu ufike mwisho juu ya biashara haramu ya
wanyama pori ambayo hupelekea wanyama pori kutoweka kwenye IKolojia.
Alisema kwa kuanza mkoa
utapanda miti ya matunda kwenye shule tano za msingi za jijini Arusha,
ambazo ni Makumbushi, Arusha school, Naura, Meru na Levolosi,na kwenye
chanzo cha maji cha Kiranyi, kutapandwa miti ya asili ambayo ni rafiki
wa mazingira ili kutunza chanzo hicho.
Alisema maadhimisho hay mwaka
huu hayataadhimishwa kitaifa bali kila mkoa kila mkoa umepewa jukumu la
kuadimisha maadhimisho hayo ambayo kli mbiu yake ya taifa inasema
tuhifadhi vyanzo vya maji kwa uhai wa taifa letu .
Kwitega, alisema katika
maadhimisho hayo wananchi na wadau watafanya usafi kwenye maeneo
mbalimbali ikiwemo soko la Kilombero, na kwenye makazi kuanzia ngazi ya
kaya ,kitongoji,kijiji,mtaa na kata ,na akatoa wito kwa kila mwananch na
taasisi mbalimbali kuhakikisha wanapanda miti kwenye maeneo yao.
Alisema siku ya kilele ya
maadhimisho hayo ya mazingira duniani,mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix
Ntibenda,(KIJIKO)ataongoza wananchi kupanda mti wa kumbukumbu kwenye
bustani ya Peace Park, iliyopo mzunguko wa Impala hotel jijini hapa .
Jun 1 at 2:32 PM
No comments:
Post a Comment