Meneja wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoa wa Ruvuma Bw. Felix Wisso. ……………………………………………………………………………………………………………
Na Zawadi Msalla- WHUSM Ruvuma
Shirika la Taifa la Hifadhi ya
Jamii( NSSF) Mkoa wa Ruvuma limeshauriwa kuinua maisha ya wasanii kwa
kuwaunganisha na mfuko huo ili kuhakikisha maisha ya wasanii
yanaboreshwa.
Akizungumza katika kikao kati ya
wadau wa sekta za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Wizara, Katibu
Mkuu wa Wizara Wizara hiyo Prof Elisante Ole Gabriel amesema kuwa
mfuko huo uangalie namna ya kukusanya wasanii na kuwaweka pamoja ili
waweze kujiunga.
“kwa upande wa wasanii wao ni
jeshi kubwa tutafute namana ya kuwasajili kama wanachama rasmi wa NSSF
ili waweza kutambulika katika ajira rasmi” alisema Prof Gabriel.
Prof Gabriel alisema kuwa
wasanii wanachangamoto nyingi zinazo wakabili ambazo zinarudisha nyuma
kada yao moja wapo ikiwa ni hiyo ya kutokuwa wanachama wa mifuko ya
Jamii.
Kwa upande wake Meneja wa NSSF
Mkoa wa Ruvuma Bw. Felix Wisso amesema lengo la mfuko huo ni kudumisha
maisha ya watanzania walio katika sekta zote hivyo basi kwa kushirikiana
na Ofisi ya Mkoa wanaangalia namna ya kuwainua wasanii hao kupitia
mikopo itolewayo na mfuko huo.
Ameongeza kuwa shirika lake
limejipanga kikamilifu kuendana na kasi ya utendaji wa Serikali ya awamu
ya tano hivyo basi elimu ya kujiunga na mfuko huo itaendelea kutolewa
kwa wananchi .
“Wasanii wanaweza kuitangaza nchi
yetu vizuri sana kama tu jamii itaamua kuwatambua na sanaa ikawa ni
ajira kamili kama ajira nyingine.”Alisema Bw. Wisso
Aidha aliwasisitiza viongozi wa
wasanii pamoja na Maafisa Utamaduni kuwahamasisha wadau wao kuingia
katika mfuko huo wa jamii kwani ni dhamana ya maisha yao.
|
June 2, 2016
NSSF YASHAURIWA KUSAIDIA WASANII
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment