Kaimu Afisa Mtendaji wa Legal Services Facility (LSF), Bi Scholastica Jullu akizungumza na waandishi wa habari jinsi wasaidizi wa kisheria wanavyosaidia kubadilisha maisha ya watanzania |
Jopo la viongozi wa LSF wakionyesha
ripoti jinsi wasaidizi wa sheria walivyotatua matatizo ya wananchi
nchini, kutoka kushoto ni Meneja Mawasiliano, Renatus Sona, Afisa Mradi
na Haki za wanawake, Bi Fortunata Kitokevya, Kaimu Afisa Mtendaji, Bi
Scholastica Jullu, wa pili kulia Meneja Ufuatiliaji na Matokeo, Juma
Mwenga na mwisho kulia ni Bw. Masele
……………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
MFUKO wa msaada wa kisheria (LSF)
umetoa ruzuku kiasi cha shilingi za kitanzania bilioni 18 kwa mashirika
yasiyo ya kiserikali yanayojishughulisha utoaji wa msaada wa kisheria
kwa ajili ya mafunzo kwa wasaidizi wa sheria 4,000 nchi nzima.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Afisa Mtendaji, Bi Scholastica Jullu
amesema kwamba ruzuku imetolewa kuanzia 2012 kwa mashirika hayo ili
kuweza kutoa mafunzo kwa wasaidizi wa sheria katika kutatua matatizo
yanayowakabili wananchi hasa wa vijijini.
“Dhumuni la uanzishwaji wa mfuko huu
ni kulinda haki za binadamu kupitia ujengaji uwezo wa kisheria na
kuongeza upatikanaji wa huduma za kisheria kwa watu masikini na
wanajamii wengine walio katika hatari ya kukosa haki zao hususani
wanawake nchini,” aliongeza Bi Jullu
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2011,
LSF imechangia katika kukuza na kulinda haki za binadamu huku ikiweka
msisitizo katika ulinzi w haki za wanawake na makundi maalum.
Amesema kwamba kutokana na mafunzo
waliopata wasaidizi wa kisheria nchini imewezesha upatikanaji wa huduma
za usaidizi wa sharia kwa watanzania takribani milioni thelathini na
tano (35 milioni).
Alifafanua kwamba katika kipindi cha
kuanzia mwaka 2013 mpaka mwaka 2015 takribani watu 90,000 walipata
huduma za msaada wa kisheria na watu 300,000 walifikiwa na elimu ya
sheria nchini nzima.
Mambo ambayo wasaidizi wengi wa
sheria wanayokutana nayo ni matatizo ya ardhi, ndoa, mirathi, watoto na
jinsi ambao asilimia 80 yalishughulikiwa na asilimia 9 tu yalipelekwa
kwenye vyombo vingine vya utoaji haki kama vile mahakama, mabaraza ya
usuluhishi, serikali za mitaa na polisi.
Bi Jullu alisisitiza mchakato
umeanza kwa wadau wa sheria, mashirika yasiyo ya kiserikali na serikali
ili kuja na sheria itakayowatambua wasaidizi wa kisheria kwenye mifumo
ya serikali.
Kwa upande wake, msaidizi wa
kisheria kutoka wilaya ya ilala, Bi Beatrice Bange amesema kwamba
changamoto kubwa ni uelewa mdogo wa watanzania wengi kuhusu huduma za
wasaidizi wa kisheria na msaada wa kisheria.
Aliongeza kwamba matatizo mengi
anayokutana nayo katika wilaya ya ilala ni ndoa, mirathi na matatizo ya
ajira kwa wafanyakazi wa kada ya chini.
Utafiti uliofanywa na shirika hilo
mwaka jana ulionyesha kuwa zaidi ya asilimia 70 ya watanzania hawana
uelewa kuhusu msaada wa kisheria na uwepo wa wasaidizi wa sheria.
|
No comments:
Post a Comment