Na Immaculate Makilika – MAELEZO
Serikali ya Tanzania yasifika kwa kuwa na uongozi unaozingatiaSheria na Utawala Bora.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es
Salaam na Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Angella Kairuki alipokuwa akifungua Mkutano wa siku
mbili wa Kimataifa kuhusu Utawala wa Sheria na Utawala bora.
Lengo la mkutano huo ilikuwa ni
kujadili masuala ya Afrika katika kukuza utawala wa sheria katika
utekelezaji wa agenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 na agenda ya
Umoja wa Afrika ya 2063.
“Mkutano huu wa kistoria nchini
Tanzania utasaidia kuleta mageuzi katika Taasisi zinazosimamia masuala
ya Sera na Sheria ambayo yatachochea maendeleo mazuri katika nchi za
Afrika”, alisema Waziri Kairuki.
Akiendelea kuzungumza Waziri
Kairuki alisema uwepo wa Marais wastaafu kama Mhe.Benjamin Mkapa na Dkt.
Jakaya Kikwete, katika mkutano huo ni ushahidi tosha wakuwepo na
mafanikio ya utawala wa sheria na utawala bora nchini Tanzania.
Kwa upande wa Rais Mstaafu
Mhe.Benjamin Mkapa, amesema ili Bara la Afrika liendelee Kiuchumi ni
lazima watu wake wapate elimu ya uraia ili waweze kushiriki zaidi katika
masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo yao pamoja na kuwepo na uongozi
utakaoleta mabadiliko “transformative leadership”.
Naye, Waziri wa Haki Sudani ya
Kusini Mhe. Pwanauwilla Unango amesema pamoja na kuwa Bara la Afrika
lina matatizo mengi kama vita, njaa, magonjwa na ndoa za utotoni, dunia
isiitazame Afrika kwa mtazamo huo pekee, bali inahitaji msaada kutoka
Jumuiya za Kimataifa.
Mkutano huo wenye kauli mbiu
“Kufikia agenda ya 2030 na agenda ya 2063:Utawala wa Sheria kwa
Maendeleo Endelevu ya Afrika”, (Achieving the 2030 agenda and agenda
2063:The rule of law as a driver of Africa’s suistainable development) ,
umeandaliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Sheria (IDLO) la
nchini Italia, kwa Ushirikiano wa Serikali ya Tanzania umehusisha wadau
mbalimbali wakiwemo Mawaziri, kutoka nchi mbalimbali za Afrika,
Mabalozi kutoka ndani na nje ya Afrika pamoja na wawakilishi wa
Mashirika ya kutetea Haki za Binadamu.
|
June 1, 2016
TANZANIA YASIFIKA KWA UTAWALA WA SHERIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment