Picha
iliyokuzwa ilichukuliwa mwaka 1974 wakati Muhammad Ali alipokuwa
akijindaa na pambano lake na George Foreman lililopigwa Kinshasa, DRC
Na Emmanuel Richard Makundi-RFI
Dunia
imealikwa kuhudhuria msiba wa Muhammad Ali, kwenye mji alikozaliwa siku
ya Ijumaa ambako maisha ya nguli huyu wa masumbwi yatasherehekewa huku
uma ukipewa nafasi ya kushiriki mazishi na ibada ya kumbukumbu, amesema
msemaji wa familia ya Ali.
Muhammad
Ali, bingwa mara tatu wa uzito wa juu duniani na mwanaharakati wa haki
za binadamu ambaye alikuwa nembo muhimu katika karne ya 20, alifariki
dunia akiwa na umri wa miaka 74 kutokana na matatizo ya kiafya
yaliyochangiwa kwa muda mrefu na mapambano yake dhidi ya ukongwa wa
kutetemeka "Parkinson.
Taarifa
rasmi kuhusu sababu za kifo cha Muhammad Ali, imeeleza kuwa alifariki
kutokana na kupata mstuko, kitaalamu inafahamika kama "Septic Shock"
ambapo hata hivyo kilichosababisha mshtuko huo hakijabainishwa
kitaalamu.
|
Mohamed Ali akiwa na mkufunzi wake Angelo Dundee
Mwanamasumbwi
huyo aliyekuwa na mbwembwe na uwezo mkubwa uliongoni, na ambaye
matamshi yake yalikuwa yanawagusa wengi, yalikuwa hatari kama ngumi
alizokuwa akizirusha uliongoni, ambapo alikimbizwa kwenye hospitali ya
Arizona mwanzoni mwa wiki iliyopita.
Wanasiasa
maarufu, wanamichezo, watu maarufu na mashabiki duniani kotea
walisimama kwa dakika moja kumkumba "Bingwa" ambaye maisha yake yameduni
kwa miongo mitatu.
Siku ya
Jumapili familia ya Ali na ndugu wa karibu, waliusinidika mwili wake
kutoka Arizona kwenda Louisville alikozaliwa kusini mwa jimbo la
Kentucky.(P.T)
Baada ya
shughuli binafsi ya kifamilia Alhamisi ya wiki hii, jeneza la Ali
litapitishwa kwenye mitaa ya Louisville siku ya Ijumaa, kabla ya
kufanyika ibada maalumu ambayo watu wote wamealikwa itakayofanyika
kwenye uwanja maalumu, ambapo rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton
anatarajiwa kusoma wasifu wa Muhammad Ali.
Msemaji
wa familia ya Ali, Bob Gunnell amewaambia waandishi wa habari kuwa,
utaratibu wa mwili wa Ali kuwekwa kwenye uwanja mkubwa unalenga kutoa
fursa kwa kila mtu atakayeshiriki kutoa heshima za mwisho kwa nguli huyu
wa masumbwi.
|
Mohamed Ali akiwa na mtoto wake wa kike aliyekuwa akipigana, Laila Ali
Bendera
kwenye mji wa Louisville zinapepea nusu mlingoti kwa heshima ya Ali,
wakati huu mashabiki wake wakifurika kwa wingi kwenye makazi ya zamani
aliyokuwa akiishi Ali ambayo sasa yamegeuzwa kuwa eneo la makumbusho,
kutoa heshima zao.
"Mioyo
yetu imeumia sana. Lakini tunafuraha kwakuwa baba yuko huru sasa,"
alisema mtoto mkubwa wa Muhammad Ali, Hana Ali kupitia mtandao wake wa
kijamii wa Twitter.
Rais wa
Marekani, Barack Obama alitoa pole kwa familia kwa mtindo ambao haukuwa
wa kawaida, kwakuwa alimzungumzia Ali, kwa yeye binafsi kama
alivyomfahamu na kwamba anazitunza kwenye chumba chake binafsi, pea
mbili za Gloves alizokuwa akizivaa, Muhammada Ali.
"Muhammad Ali alikuwa bingwa wa mabingwa, huo ndio ukweli," alisema rais Obama.
|
Mohamed Ali akiwa na watoto wake, Laila na Hana, tarehe 19 December 1978.
"Mapambano
yake nje ya ulingo yalimgharimu mikanda yake na imani kwa uma. Ingeweza
kumtengenezea maadui, kushoto na kulia na hata kukaribia kuswekwa jela,
lakini Ali alisimamia kile alichoamini," aliongeza rais Obama.
Katika
hali ya kawaida kabisa, Bill Clinton ambaye atasema neno kuhusu Ali
wakati wa ibada ya mazishi, yeye pamoja na mke wake Hillary anayewania
kuteuliwa na chama chake kuwania urais wa Marekani, wamesema Ali,
alikuwa kiungo muhimu cha uzuri na baraka, kasi na nguvu ambavyo kamwe
haviwezi kulinganishwa,"
Ali alipelekwa hospitali ya Phoenix mwanzoni mwa juma, lakini hali yake ilibadilika ghafla na kuanza kuzorota.
Muda wake wa mwisho, Ali aliutumia akiwa amezungukwa na familia yake na kwamba hakuumia.
Ali
amekuwa akiishi kwenye mji wa Phoenix na mkewe Lonnie, akiwa ni mke wa
nne aliyemuoa mwaka 1986, alifanikiwa kuwa na wajukuu tisa, watoto
wakike saba na wawili wa kiume.
Msemaji wa familia ya Ali, amesema kuwa bindio huyo kwa sehemu kubwa ndiye aliepanga utaratibu wa namna atakavyombolezwa.
|
No comments:
Post a Comment