Mwanamke mmoja mwandishi wa habari ameuawa kwenye mji mkuu wa Somalia Mogadishu.
Sagal Salaad Osman, ambaye alikuwa akifanya kazi na kituo cha serikali aliuawa na watu waliokuwa wamejihami na bastola.
Somalia
ni moja ya nchi hatari zaidi duniani kwa waandishi wa habari, lakini
kuuawa kwa waandishi wa habari wa kike si jambo la kawaida.
Hakuna
kundi lililodai kutekeleza mauaji hayo, lakini huenda yametekelezwa na
kundi la al Shabaab ambalo mara nyingi huwalenga waandishi wa habari.BBC
|
No comments:
Post a Comment