Imeelezwa
kuwa gharama kubwa za usafiri wa anga nchini zitapungua pale Serikali
itakapoliwezesha Shirika la ndege Tanzania (ATCL), kuwa na ndege zake.
Akizungumza
mara ya kukagua kiwanja cha ndege cha Nduli Mkoani Iringa Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema kwa mwaka
wa Fedha 2016/17 kiasi cha bilioni 500 kimetengwa kwa ajili ya ununuzi
wa ndege tatu.
“Nauli
za usafiri wa anga zitashuka hivi karibuni pale ndege tatu
tulizoziagiza zitakapoanza kutoa huduma ya Usafiri hapa nchini hivyo
niwatoe hofu watumiaji wa usafiri wa anga,” amesema Profesa Mbarawa.
Prof.
Mbarawa amemuagiza Meneja Uwanja wa ndege wa Nduli Mkoani Iringa Bi.
Hana Kibupile kuhakikisha kwamba uwanja wa ndege wa Iringa unafanya kazi
katika viwango vinavyokubalika kimataifa ili kuvutia wasafiri wengi
wanaoelekea Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kutumia uwanja huo na hivyo kukuza
uchumi wa Iringa.
“Uwanja
wa ndege wa Iringa ni miongoni mwa viwanja 11 ambavyo tutavifanyia
ukarabati hivi karibuni hivyo jukumu lenu ni kutoa huduma inayokidhi
viwango,” amesisitiza Prof. Mbarawa.
Waziri
huyo wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano amesema Serikali itaupanua
uwanja wa ndege wa Iringa hivyo wote waliovamia eneo la uwanja huo
waondoke mara moja kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa dhidi yao na
wale watakaochukuliwa maeneo yao Serikali itawafidia.
Naye
Meneja wa uwanja wa ndege wa Iringa Bi. Hana Kibupile amemuomba Waziri
Prof. Mbarawa kuupa uwanja huo gari jipya la zimamoto ili kuuwezesha
uwanja huo kufanya kazi katika viwango vinavyokubalika.
Idadi
ya abiria wanaotumia uwanja wa ndege wa Nduli imeongezeka kutoka abiria
4405 mwaka 2011 hadi 8375 mwaka 2015 na hivyo kuongeza uchumi wa Mkoa
wa Iringa.
Katika
hatua nyingine Prof. Mbarawa amekagua barabara ya Iringa –Kilolo yenye
urefu wa KM 35 na kusisitiza kwamba Serikali imepanga kujenga barabara
hiyo kwa kiwango cha lami kwa KM 28 zilizobaki.
|
June 7, 2016
NAULI ZA USAFIRI WA ANGA NCHINI KUPUNGUA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment