Katibu
Mkuu Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Prof. Adolph Mkenda
amesema kuwa serikali imeondoa tozo ya uhakiki wa viwango vya ubora na
usajili katika kuanzisha viwanda vidogovidogo katika shirika la viwango
Tanzania(TBS) ambao sasa unafanyika bure.
Prof
Mkenda ameyasema hayo alipokuwa akitoa mada katika uzinduzi wa Jukwaa
la kuwezesha wanawake na akaunti ya mkopo ya MALAIKA ambayo imeanzishwa
katika benki ya Wanawake Tanzania.
Aidha
amesema ameagiza kwa wilaya na vijiji kuanzisha viwanda kwani kwa
kufanya hivyo watakuwa wanaunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya
Tano na kuinua uchumi wa nchi yetu.
“Bidhaa
za kilimo kwa sasa zinapewa dhamana na hivyo basi nawaimiza wanawake
waanzE kuanzisha viwanda vidogovidogo kwani uanzishwaji wake ni bure,”
alisema Prof Mkenda.
Pia
alisema kuwa kipato cha kati nchini kinaongezeka siku hadi siku na
kuwataka wanawake kutolima kwa mazoea na kuwataka wafanye biashara kwa
faida kwa kutumia teknolojia sahihi ili kuongeza uzalishaji.
Katika
upande mwingine aliwataka wanawake kutokata tamaa katika kujiinua
kiuchumi kwani Serikali ya awamu ya tano iko makini na inaweka mazingira
mazuri kwa wanawake kama kuondoa tozo zisizokuwa za lazima ili kuvutia
wawekezaji wa viwanda vidogo vidogo.
Katika
uzinduzi huo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Bi Samia
Suluhu Hassan alizindua jukwaa hilo na akaunti ya mikopo ya wanawake ya
MALAIKA kupitia benki ya wanawake ambayo akaunti hiyo itakuwa na mikopo
yenye riba nafuu ya asilimia 5 kwa muda wa miezi sita,mafunzo
yanatolewa bure,hamna haja ya kuleta mchanganuo wa mahesabu na hakuna
hitaji la dhamana yenye lengo la kuwakwamua wanawake kiuchumi.
Na Daudi Manongi-MAELEZO
|
June 7, 2016
SERIKALI YAONDOA TOZO YA UHAKIKI NA USAJILI WA VIWANDA VIDOGO VIDOGO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment