Katika
kuhakikisha kila Mtanzania anapata elimu kuhusu Malengo 17 ya Maendeleo
Endelevu (SDGs) ambayo yanatakiwa kumfikia mtu mmoja mmoja, ofisi ya
Umoja wa Mataifa nchini (UN) imetoa mafunzo kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu
cha Dodoma (UDOM), mafunzo ambayo yataweza kuwajengea uwezo kuhusu
mpango huo na jinsi unavyoweza kubadili maisha yao.
Akizungumza
na MO blog kuhusu mafunzo hayo, Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa
Mataifa (UN) nchini, Bi. Hoyce Temu alisema kuwa mafunzo hayo ni sehemu
ya juhudi ya Umoja wa Mataifa (UN) kuwezesha uelewa kwa tumaini
kuwafanya wananchi hasa vijana kutambua wajibu wao katika kutekeleza
malengo hayo.
Alisema
katika mafunzo hayo wametoa elimu kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu
(SDGs) kwa wanafunzi zaidi ya 200 na hayo siyo mafunzo ya kwanza kwani
wameshatoa mafunzo kama hayo kwa wabunge wa Tanzania lakini pia
wameshafanya mafunzo kama hayo jijini Arusha ambapo yalihudhuriwa na
vijana zaidi ya 200.
“Tunataka
kila Mtanzania ajue kuhusu Malengo ya Maendeleo Eendelevu (SDGs)
tumeshatoa elimu sehemu nyingine hii siyo ya kwanza na tutaendelea
kwenda maeneo mengine kutoa elimu zaidi na katika hilo ofisi ya Umoja wa
Mataifa nchini ipo imejipanga kufanya hivyo,” alisema Bi. Temu.
|
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendesha semina
fupi kuhusu Malengo 17 mapya ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa wanafunzi
wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) (hawapo pichani) inayoendelea mjini
Dodoma chuoni hapa.
Nae
Mkuu wa Kitovu cha Mitaala katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof.
Willy Komba alisema mafunzo hayo yamewajenga na kupata elimu ambayo
walikuwa hawajaipata awali inayohusu Malengo ya Maendeleo Endelevu
(SDGs) na pia kueleza kutokana na umuhimu wake watakaa kuangalia ni
jinsi gani wataweka katika mtaala wa masomo ili wanafunzi wajifunze
kuhusu SDGs.
“Sababu
na mimi ndiyo Mkuu wa kitengo cha mitaala nitakaa na wenzangu tuone
jinsi gani tunaweza kuweka katika mitaala yetu ili hata wanafunzi
wajifunze kama masomo, tunawashukuru kwa mafunzo yenu mmetupa changamoto
mpya ambayo hatukuwa nayo,” alisema Komba.
|
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, ambaye pia ni mmoja wa wakufunzi wa masuala ya SDGs, Hoyce Temu akifafanua jambo wakati wa semina fupi ilihusisha wanafunzi wa UDOM inayoendelea mjini Dodoma. |
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wanafunzi wa UDOM wakati wa semina fupi kuhusu Malengo ya dunia iliyoandaliwa na Umoja huo mjini Dodoma jana. |
Mkuu wa Kitovu cha Mitaala katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof. Willy Komba akitoa neno la shukrani kwa Umoja wa Mataifa kwa kuwapatia mafunzo ya SDGs mara baada ya kumalizika semina fupi kwa wanafunzi wa UDOM. |
Kutoka kushoto ni Waziri wa Habari wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), James Msofe, Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, ambaye pia ni mmoja wa wakufunzi wa masuala ya SDGs, Hoyce Temu na Mwanafunzi wa mwaka wa tatu UDOM wa Didgrii ya kwanza ya Mifumo ya Upashanaji Habari, Lobezi Kulilo katika picha kumbukumbu wakilishilia mabango ya SDGs. |
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa UDOM mara baada ya kumalizika kwa semina kuhusu Malengo ya Dunia iliyoandaliwa na Ofisi ya Umoja Mataifa mjini Dodoma jana. |
No comments:
Post a Comment