Jinamizi
la kashfa ya uchotwaji fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow bado
linamsumbua mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka baada
ya kuliibua kwenye semina ya mapambano dhidi ya ufisadi, akichongea
wabunge ambao hawajaguswa.
Profesa
Tibaijuka alipoteza uwaziri wa nyumba, ardhi na makazi kwenye sakata
hilo baada ya kubainika kuwa aliingiziwa fedha zinazoonekana zilitoka
kwenye akaunti hiyo iliyokuwa inamilikiwa kwa pamoja na Tanesco na
kampuni ya kufua umeme ya IPTL.
Profesa
Tibaijuka alikuwa mmoja kati ya viongozi wa ngazi ya waziri, mbunge,
jaji na viongozi wa dini walioingiziwa fedha ambazo zinatokana na Sh306
bilioni zilizochotwa kwenye akaunti hiyo.
Akichangia
katika semina hiyo inayolenga kuwajengea wabunge uwezo wa kupambana na
ufisadi na ambayo iliandaliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Ufisadi
(ACFE), Profesa Tibaijuka alisema wakazi wa jimbo lake walimchagua kwa
mara nyingine licha ya tuhuma za Escrow kwa sababu hawakuziamini.
Alisema
fedha hizo za Escrow zilitoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kwenda
benki ya Stanbic na Mkombozi, lakini cha ajabu majina ya watu waliopewa
fedha kupitia benki moja yalitolewa na yale ya benki nyingine
yalifichwa.
Alisema inakuwaje yeye anakuwa katika tuhuma, wakati aliyempa fedha hizo hatuhumiwi.
Watu
waliotajwa kwenye sakata hilo ni wale waliopewa fedha zilizopitia benki
ya Mkombozi, lakini hadi sasa wale waliopewa fedha zinazodaiwa kuwa ni
taslimu kutoka Stanbic hawajatajwa.
Alisema
sheria pekee yake haiwezi kufanya lolote katika mapambano dhidi ya
ufisadi na hakubaliani na wabunge wanaosema kuwa hata kama mahakama
imeshindwa kuthibitisha ufisadi, watuhumiwa wataifishwe mali zao.
“Sisi wabunge hatukuja kufanya kazi hiyo, tumekuja kutunga sheria ili zisaidie katika kutuongoza,” alisema.
“Ni vyema kuzungumzia unyofu wa watu kwa kuanzia katika shule, makanisa, misikiti na wabunge.”
Aliituhumu Takukuru kuwa inakubali kutumiwa kwa kuchagua kesi za kuchunguza.“Tume ya Maadili ndio usiseme,” alisema.
“Mie
nimeshawahi kushtakiwa Tume ya Maadili, najua kuwa kuna mbunge mwenzetu
hapa alipata fedha za Escrow, lakini kwa sababu hakuwa mzungumzaji
ameondoka bungeni wala hakuna mtu anajua kama alipata. Unaona jinsi
ambavyo hawa watu hawako makini,” alisema.
Mbunge
wa Hanang (CCM), Dk Mary Nagu alilia na watu aliowaita wazushi kwamba
wanawazushia wenzao kuchukua rushwa wakati hakuna ukweli.
|
June 3, 2016
PROFESA TIBAIJUKA:WAPO WALIOCHOTA FEDHA ZA ESCROW LAKINI WAMENYAMAZIWA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment