Na Fatma Salum- MAELEZO.
Dodoma
Serikali imeagiza kuwa kuanzia
Mwezi Julai mwaka huu ni lazima mfumo wa kielektroniki utumike katika
utoaji wa risiti kwa tozo, faini, ada na malipo mengine yote ya Serikali
Kuu, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Wakala wote wa Serikali ili
kudhibiti upotevu wa mapato.
Agizo hilo limetolewa na Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango wakati akiwasilisha hotuba
ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha
2016/2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
Dkt. Mpango alisema kuwa agizo
hilo pia linahusisha malipo ya faini za mahakamani, faini za usalama
barabarani, viingilio kwenye mbuga za wanyama na vibali vya kuvuna
maliasili.
“Naziagiza ofisi zote za Serikali
kutoa risiti za kielektroniki kwa malipo yote yatakayofanyika kwani
matumizi ya vifaa na mifumo ya kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato
yataongeza ufanisi na kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali.” Alisema
Dkt. Mpango.
Katika kufanikisha hilo Dkt.
Mpango aliongeza kuwa Maafisa Masuuli wote wanaelekezwa kusimamia
ipasavyo utekelezaji wa agizo hilo.
Katika hatua nyingine, Dkt.
Mpango alisema kuwa Serikali imeamua kufanya uthamini wa majengo kwa
mkupuo ili kuongeza mapato yatokanayo na kodi ya majengo na usimamizi
wake utakuwa chini ya Mamlaka ya Mapato Tanzania.
Katika hotuba hiyo Dkt. Mpango
amefafanua mkakati wa Wizara yake kusimamia kikamilifu utekelezaji wa
Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano kuanzia 2016/17 hadi 2020/21
ambao umejikita katika kujenga msingi wa uchumi wa viwanda na maendeleo
ya watu.
|
June 1, 2016
SERIKALI YAZIAGIZA TAASISI ZAKE KUTOA RISITI ZA KIELEKTRONIKI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment