KAMATI ya Utendaji ya Chama cha
Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) imemteua Makamu
Mwenyekiti wa TASWA, ambaye pia Mhadhiri Msaidizi wa Shule Kuu ya
Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam (UDSM), Egbert Mkoko kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo za
Wanamichezo Bora Tanzania mwaka 2015/2016.
Pia TASWA imeteua wajumbe tisa
wa kamati hiyo. Majina yao na vyombo vyao katika mabano ni Mahmoud
Zubeiry (Bin Zubeiry Sports- Online), Jane John (TBC), Baruani Muhuza
(Azam Media), Limonga Justine (Redio Uhuru), Maulid Kitenge (E-FM
Redio), Deogratias Rweyunga (Redio One/ITV), Shaffih Dauda (Clouds
Media), Asha Muhaji (Bingwa) na Nelly Mtema (Daily News).
Kamati inaweza kuongeza wajumbe
wengine au kupunguza kwa kadri itakavyoona inafaa. Utaratibu wa
kuizindua kamati hiyo unaandaliwa na sekreterieti ya TASWA. Jukumu la
kamati itakuwa ni kuandaa utaratibu wa kuwapata wanamichezo watakaowania
tuzo hiyo na pia kuteua washindi kwa kila mchezo.
Tuzo za Wanamichezo Bora
zinazotolewa kila mwaka na TASWA zimepangwa kufanyika Agosti 26, mwaka
huu, Dar es Salaam zikihusisha michezo mbalimbali.
B; ZIARA YA MAFUNZO NAIROBI
TASWA kwa kushirikiana na Chama
cha Waandishi wa Habari za Michezo Kenya, vimeanzisha program ya ziara
ya mafunzo na kubadilishana uzoefu baina ya vyama hivyo viwili, ikiwa
katika makundi tofauti ya wahariri/waandishi waandamizi na kundi lingine
la waandishi wa habari chipukizi.
Kwa kuanzia wahariri wa habari
za michezo 18 au wale wenye uzoefu katika uandishi usiopungua miaka kumi
kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wataenda Nairobi kwa ziara
ya mafunzo kuanzia Julai 6-9 mwaka huu.
Tunaamini wakirudi wataendelea kuwa waalimu wazuri kwa wale chipukizi, ambao nao watapata fursa kama hiyo siku za usoni.
Ahsanteni,
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
01/06/2016
|
June 1, 2016
TAARIFA KUTOKA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO (TASWA)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment