Frank Mvungi-Maelezo
Wakala wa Taifa wa Utafiti wa
Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) umeanza kufanya utafiti
utakaosadia kupunguza kiwango cha Hewa ya Ukaa (green house gases)
kinachozalishwa kutokana na shughuli za ujenzi ili kupunguza uharibifu
wa mazingira.
Akizungumza na Waandishi wa
Habari leo jijini Dar es salaam Mhandisi Heri Hatibu kutoka wakala huo
amesema utafiti utasaidia kupunguza gharama za Ujenzi hapa nchini.
Akizungumzia Malengo ya Utafiti
huo Hatibu amesema kuwa, utasaidia kupunguza kiwango cha nishati
kinachotumiwa kwenye nyumba kwa ajili ya kupooza hewa hivyo kuokoa fedha
inayoweza kutumika kufanya mambo mengine.
“Sekta ya Ujenzi inachangia
asilimia 40 ya hewa ya ukaa hivyo lengo la utafiti huu ni kusaidia
kuondoa tatizo hili mara baada ya utafiti wetu kukamilika.” Alisisitiza
Mhandisi Hatibu.
Aidha Hatibu amesema kuwa,
utafiti huo utawezesha kusanifu majengo yatakayotumia nishati kidogo
kwenye hatua ya ujenzi na hata wakati wa matumizi ya majengo husika. Pia
utachochea matumizi ya vifaa vya Ujenzi vinavyopatikana katika maeneo
ya karibu na shughuli za ujenzi.
Pia utafiti huo utasaidi kutoa
elimu kwa wadau wa ujenzi kuhusu nishati mbadala katika kutekeleza
shughuli za ujenzi, ikiwemo kuacha kukata miti.
Vile vile wananchi wataelimishwa
kuhusu njia bora za uchomaji wa matofali ili waweze kutumia vifaa
vingine badala ya kukata miti kwa ajili ya uchomaji matofali.
Matokeo ya utafiti huo
unaotarajiwa kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka huu yatasaidia wadau wa
sekta hii kupanga mipango ya ujenzi itakayosaidia kupunguza athari
katika mazingira zinazosababishwa na matumizi makubwa katika uzalishaji
vifaa vya ujenzi na hata katika ujenzi.Utafiti huo unafanyika katika
Mikoa ya Dar es salaam, Dodoma, Morogoro na Tanga.
|
June 1, 2016
TATIZO LA HEWA YA UKAA KUPUNGUA HAPA NCHINI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment