Na: Lilian Lundo – MAELEZO
Askofu wa Kanisa la Good News for
All Ministry Dkt. Charles Gadi amewapa siku tatu walioficha sukari
kuitoa na ikiwa watakaidi agizo hilo basi ardhi iwakatae.
Askofu Gadi ameyasema hayo leo
jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya
uhaba wa sukari nchini na maandalizi ya mkutano wa kumuombea Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utakaofanyika jiji la Arusha.
“Tanzania haina tatizo la sukari
bali sukari ziko kwenye maghala, wafanyabiashara wamezificha ili waje
kuuza kwa bei ya juu. Tunamuomba Mungu ili watu hao ardhi iwakatae ikiwa
hawatatoa sukari ndani ya siku ya tatu,”alisema Askofu huyo.
Pia, Askofu Gadi ametoa wito kwa
wafanyabiashara kuacha tabia ya kuficha sukari na wakumbuke kuwa waislam
wapo katika maandalizi ya kutimiza nguzo muhimu ya imani ya dini yao
ambapo wataanza mwezi wa Ramadhani na watahitaji sukari kwa ajili ya
kuandaa futari.
Vile vile Askofu huyo ameiomba
Serikali kuagiza sukari kwa wingi ili waumini wa dini ya Kiislam waweze
kutimiza kwa urahisi nguzo ya mwezi wa Ramadhani.
Aidha, akizungumzia juu ya
mkutano wa maombi utakaofanyika jiji la Arusha, Askofu Gadi amesema kuwa
mkutano huo ni maalum kwa ajili ya kumuombe Rais Dkt. John Pombe
Magufuli ili aweze kufanikiwa katika nia yake ya kujenga upya uchumi,
uadilifu na ustawi wa Tanzania.
Mkutano huo unategemewa kufanyika
siku ya Jumatano Juni 08, 2016 kuanzia 4 asubuhi mpaka saa 12 jioni
viwanja vya relini, ambao umeandaliwa na Kanisa la Good News for All
Ministry kwa kushirikiana na Umoja wa Makanisa ya Arusha.
|
June 2, 2016
WALOFICHA SUKARI ARDHI IWAKATAE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment