Meneja habari, elimu na Mawasiliano wa Wakala wa Serikali Mtandao(eGA) Bibi. Suzan Mshakangoto akiongea na waandishi wa habari na wafanyakazi wa taasisi hiyo hawapo pichani kuhusu ushiriki wa Taasisi za kiserikali katika kupanga na kutekeleza miradi ya TEHAMA Serikalini uliofanyika leo jijini Dar es salaam. |
Meneja habari, elimu na
Mawasiliano wa Wakala wa Serikali Mtandao(eGA) Bibi. Suzan Mshakangoto
katikati akiongea na waandishi wa habari na wafanyakazi wa taasisi hiyo
kuhusu ushiriki wa Taasisi za kiserikali katika kupanga na kutekeleza
miradi ya TEHAMA Serikalini uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Picha zote na Ally Daud-Maelezo
………………………………………………………………………………………….
Na: Frank Shija, MAELEZO
Ofisi naTaasisi za umma
zashauriwa kushirikiana naWakala wa Serikali Mtandao (eGA) katika
kupanga na kutekeleza miradi mbalimbali ya Tehama.
Ushauri huo umetolewa na Meneja
wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA)
Bibi. Suzan Mshakangoto wakati akiongea na waandishi wa habari leo
jijini Dar es Salaam.
Bi. Mshakangoto amebainisha kuwa
kumekuwapo na changamoto ya Taasisi za umma kuanzisha miradi ya TEHAMA
inayofanana huku zikiwa na taarifa zinazokinzana na kuisababishia
gharama zisizo za lazima Serikali.
Aidha alisema kuwa ili
kujiridhisha na miradi ya TEHAMA Wakala hiyo imeweka vigezo katika
Orodha hakiki ya miradi ya TEHAMA Serikalini, inayopatikana katika
tovuti ya Wakala ili uweze kuhakikiwa na kuthibitishwa.
“Kutokana na utaratibu huo kuleta
changamoto mbalimbali,taasisi yeyote ya umma inatakiwa kuwasilisha
mradi wake kwaWakalaya Serikali Mtandao ukiwa unaendana na vigezo
vilivyowekwa katika orodha ya miradi ya TEHAMA Serikalini inayopatikana
katika tovuti ya wakala ambayo ni www.ega.go.tz” AlisemaBi. Suzan.
Changamoto zinazojitokeza
kutokana na utaratibu huo ni pamoja na kutofautiana kwa taarifa ya aina
moja kutoka taasisi tofauti akitolea mfano wa Rita wanaweza kuwa na Jina
la Juma Hassan na mtu yulelyule ukienda Bima ya Afya anaitwa Juma
Kassim Hassan.
Kutokana na mkanganyiko huo na
Wakala inashauri na kuzitaka taasisi zote za Serikali kuwasilisha andiko
la miradi yao ya Tehama kwa Wakala ya Serikali Mtandao ili kuhakikiwa
kama zinakidhi vigezo, malengo na dira ya maendeleo ya Serikali ya mwaka
2025 na kama mradi huo niendelevu.
Aidha wito umetolewa kwa
wafanyabiashara wanaojihusisha na miradi au utengenezaji wa mifumo ya
Tehama Serikalini kujiridhisha kama miradi waliyokusudi kuitekeleza
inakidhi vigezo vya kuanzisha miradi ya TEHAMA kama vilivyoainishwa
katika orodha ya miradi ya Tehama Serikalini.
Wakala wa Serikali Mtandao (eGA)
ni taasisi ya Serikali kwa mamlaka iliyonayo kisheria inawajibika
kusimamia na kuratibu masuala yote yanayohusu Serikali Mtandao hivyo ni
wajibu wake inapoona mambo yanaenda kinyume na taratibu na miongozo ya
usimamizi wa miradi ya Tehama Serikalini.
Na: Frank Shija, MAELEZO
02/06/2016

|
No comments:
Post a Comment