Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto), Mhe. Margaret Sitta Mbunge wa Urambo (katikati) na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura wakielekea ndani ya Ukumbi wa Bunge, Dodoma leo. |
Mchezaji wa kulipwa wa mpira wa kikapu nchini Marekani kutoka Tanzania Hasheem Thabeet (kulia) akiwa na baadhi ya wageni mbalimbali waliolitembelea Bunge leo. |
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson (kulia) akisalimiana na Meneja wa VETA mkoa wa Iringa Bw. Maganga nje ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.Katikati ni Mbunge wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto. |
Baadhi ya Wabunge na Mawaziri wakifuatilia masuala mbalimbali ndani ya ukumbi wa Bunge wakati wa kikao cha 35 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo. |
Mchezaji wa kulipwa wa mpira wa kikapu nchini Marekani kutoka Tanzania Hasheem Thabeet (kushoto) akifurahia jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju (wa pili kutoka kushoto) na baadhi ya Wabunge nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma. |
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimsisitiza jambo Meneja wa VETA mkoa wa Iringa Bw. Maganga nje ya Ukumbi wa Bunge Dodoma. |
Mbunge wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto (wa pili kutoka kulia), Mbunge wa Mtera Mhe. Livingstone Lusinde (wa tatu kutoka kulia) na Mbunge wa Geita vijijini Mhe. Joseph Kasheku Msukuma ( pili kutoka kushoto)wakimweleza jambo Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe nje ya Ukumbi wa Bunge leo. |
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Mhe. William Lukuvi (Kulia) akizungumza jambo na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni leo mjini Dodoma.Picha na Aron Msigwa na Fatma Salum–MAELEZO, DODOMA. |
No comments:
Post a Comment