Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akikabidhiwa kitabu cha picha za wanyamapori waliopo katika Pori la Akiba la Selous na Mtaalamu wa picha wa Kimataifa, Bw. Robert Ross wakati alipomtembelea leo ofisini kwake Mpingo House jijini Dar es Salaam. Kitabu hicho cha picha za wanyamapori waliopo katika pori la Akiba la Selous kinatarajiwa kuzinduliwa leo na Mhe. Waziri ambaye atawakilishwa na Naibu Katibu Mkuu , Injinia Angelina Madete, katika Hoteli ya Slip way. Kitabu hicho kinatarajiwa kutumika kama nyenzo muhimu katika kutangaza Utalii wa Tanzania katika Nyanja za Kimataifa. |
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akiangalia baadhi ya picha katika kitabu cha picha za wanyamapori waliopo katika Pori la Akiba la Selous na mara baada ya kukabidhiwa kitabu hicho na Mtaalamu Kimataifa, Bw. Robert Ross (kushoto) wakati alipomtembelea leo ofisini kwake Mpingo House jijini Dar es Salaam. Kitabu hicho cha picha za wanyamapori waliopo katika pori la Akiba la Selous kinatarajiwa kuzinduliwa leo jioni katika Hoteli ambapo Kitabu hicho kitakuwa ni nyenzo muhimu katika kutangaza Utalii wa Tanzania katika Nyanja za Kimataifa. |
Huu ni mwonekano wa nje wa kitabu cha Picha zilizochukuliwa katika Pori la Akiba Selous na Mtaalamu wa picha wa Kimataifa, Bw. Robert Ross, Kitabu hicho kinatarajiwa kuzinduliwa leo na Waziri, Prof. Maghembe ambaye atawakilishwa na Naibu Katibu Mkuu Injinia Angelina Madete katika hoteli ya Slipway. |
No comments:
Post a Comment