Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January
Makamba ametoa wito kwa Wananchi wa Kata ya Mbweni kutunza mazingira na
kutoa kipaumbele kwa mazingira.
Mh. Makamba liyasema hayo wakati wa zoezi la upandaji mikoko lilifanyika katika fukwe za bahari ya Hindi zilizoko Mbweni.
Akiongoza
Wananchi wa Kata hiyo kupanda miche 5,000 ya mikoko , Waziri Mkamba
alisititiza pia wanafunzi wa shule waliopo katika eneo hilo kupenda
mazingira yao na kuyatunza ili yawafae baadaye.
Wakisoma
Risala yao, wanawake wa Mbweni walimuomba Waziri awasaidie kuwapatia
vitendea kazi kwa ajili ya kuhudumia mikoko pamoja na kumuomba awasaide
kuwatatulia changamoto wanazokutana nazo. Ikiwamo ya maafisa wa TRA
kukata hovyo mikoko wanapokua wanafanya doria katika fukwe za Mbweni.
Aidha
Waziri aliwahukuru wananchi wa Mbweni waliojitokeza kujumuika naye
katika zoezi hilo la upandaji mikoko. Shughuli za upandaji mikoko ni
kuelekea maadhimisho ya siku ya mazingira ambayo kilele chake ni Juni, 5
kila mwaka.
|
June 6, 2016
WAZIRI MAKAMBA AWATAKA WANANCHI KUTUNZA MAZINGIRA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment