KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

July 21, 2016

ALI KIBA BARAKA DA PRINCE WAVAMIWA NA MAJAMBAZI SOUTH AFRICA,MAZITO YASEMWA


Taarifa kuhusu waimbaji wa muziki wa bongoflevaAlikiba na Baraka Da Prince ambao wote wako chini ya lebo ya Rockstar 4000, kuvamiwa na Majambazi wenye silaha Afrika Kusini saa tatu usiku kwa saa za Afrika Mashariki July 20 2016.
Management inayowasimamia imeiambia kwamba wawili hawa pamoja na watu wengine wakati wanavamiwa, walikua kwenye eneo kulikofanyika kikao cha maandalizi ya kazi zilizowapeleka Afrika Kusini kwa siku saba.
Majambazi hao walikua sita na walikua pia na silaha za moto (bunduki)
Miongoni mwa vitu walivyoibiwa ni pamoja na simu zao za mkononi ambapo Majambazi hao wakati wote wa tukio waliwanyooshea Bunduki kina Alikiba kuwatisha zaidi na bila kutaka kupoteza muda.
Baraka Da Prince na Alikiba wote ni wazima wa afya na hawakurudhika na chochote kwenye hilo tukio
Pamoja na tukio hili kutokea, Baraka na Alikiba hawatosimama kufanya projects zao… wamechukua mapumziko mafupi na kisha wataendelea.

CHANZO:BLOG YA WANANCHI

No comments:

Post a Comment