Rais
Dk. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
Taifa Mh. Dk. Jakaya Kikwete wakati akifungua kikao cha Kamati Kuu ya ya
Halmashauri kuu ya CCM kilichofanyika leo Makao Mkuu ya CCM Dodoma
kupendekeza jina la Mwenyekiti mpya wa CCM ambapo jina hilo litapelekwa
kwenye Halmashauri Kuu ya Taifa kwa ajili kupelekwa kwenye mkutano
mkuu na kuthibitishwa katika Mkutano Mkuu maalum wa CCM unaotarajiwa
kufanyika Julai 23 mwaka huu mjini Dodoma, Katikati ni Makamu Mwenyekiti
wa CCM Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi Taifa Mh. Dk. Jakaya Kikwete akifungua kikao
cha Kamati Kuu ya ya Halmashauri kuu ya CCM kilichofanyika leo Makao
Mkuu ya CCM Dodoma Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip
Mangula na katikati ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurrahman Kinana.
Rais
Dk John Pombe Magufuli kushoto pamoja na Mwenyekiti wa CCM Dk Jakaya
Kikwete na viongozi wengine wakiimba wimbo maalum wa CCM wakati mkutano
huo uliofanyika leo Makao Mkuu ya CCM Dodoma
Mjumbe
wa Kamati Kuu Ndugu William Lukuvi akizungumza na wajumbe wenzake Adam
Kimbisa kushoto na Nape Nnauye Katibu Mwenezi wa CCM Taifa.
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM Adam Kimbisa akuzungumza na wajumbe wenzake
kutoka kushoto ni Nape Nnauye Katibu Mwenyezi wa CCM Taifa, Mama Zakia
Megji , William Lukuvi na Mohamed Seif Khatib.
Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa akisalimiana na Wajumbe wa kamati kuu wakati alipowasili kuhudhuria katika mkutano huo.
Wajumbe
wa Kamati Kuu Mzee Steven Wasira kulia na Msemaji wa CCM Christopher
Ole Sendeka wakifurahia jambo kabla ya mkutano huo kuanza.
 |
Mjumbe wa Kamati kuu kutoka Zanzibar Sadifa
Juma Khamis akizungumza na mjumbe mwenzake Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Wazazi CCM Ndugu Abdallah Bulembo kutoka kulia ni Jerry Silaa na Hussein
Mwinyi. |
No comments:
Post a Comment