|
Balozi
Ombeni Sefue akizungumza na Menejimenti ya Wakala wa Taifa wa Utafiti
wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) wakati
alipofanya ziara katika taasisi hiyo mwishoni mwa wiki ili kujionea
shughuli mbali mbali zinazofanywa na taasisi hiyo , Kwa kiwango
kikubwa (NHBRA) imeonyesha ni taasisi inayoweza kujenga nyumba za bei
nafuu sana hasa vijijini ili watanzania wa maeneo hayo waweze kupata
makazi bora ya kuishi kwa bei rahisi zaidi, Kulia katika picha ni
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Bw.Matiko Samson Mturi. |
|
Mkurugenzi
Mtendaji wa taasisi hiyo Bw.Matiko Samson Mturi akizungmza wakati
alipokuwa akimkaribisha Balozi Ombeni Sefue wakati alipotembelea katika
taasisi ya Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba na Vifaa vya Ujenzi
NHBRA Mwenge jijini Dar es salaam. |
Taasisi hiyo pia imekuwa
ikijihusisha na mafunzo teknolojia ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu
kwa vikundi mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na kuwafundisha juu ya
utengenezaji wa matofali, vigae vya kuezekea nyumba pamoja na ujenzi wa
nyumba za zenyewe ambapo taasisi na wananchi mbalimbali wanaweza
kufaidika na mpango huo nchini.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES
SALAAM)
|
Bw.
Sylivester Shumbusho Fundi kutoka Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba
na Vifaa vya Ujenzi NHBRA akimpa maelezo Balozi Ombeni Sefue juu ya
utengenezaji wa matofali ya bei rahisi kwa kutumia udongo wakati
alipokuwa akitembelea karakana ya taasisi hiyo iliyopo Mwenge jijini Dar
es salaamKatikati ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bw. Matiko Samson
Mturi. |
No comments:
Post a Comment