Mkuu wa biashara wa AMANA BENKI Bw. Munir Rajab akifafanua jambo kuhusu kituo hicho.
NA SELEMANI MAGALI- DARESLAAM
BENKI ya
Kiislamu ya Amana imezindua kituo chake kipya cha huduma kwa wateja kwa
njia ya mawasiliano ya simu ikiwa ni sehemu ya mkakati wao wa kuboresha
huduma kupitia teknolojia ya mawasiliano
Akizungumza
na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam,Meneja Mwandamizi Huduma
kwa wateja wa Benki hiyo Bw. Juma Msabaha alisema uzinduzi wa kituo
hicho umelenga kuboresha mahusiano ya wateja pamoja na kusogeza huduma
za kibenki karibu na wananchi.
Akifafanua
kuhusu kituo hicho, Bw. Msabaha alisema kituo hicho kitafanya kazi kwa
masaa 15 kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa nne usiku ambapo wateja wa
Amana na ambao bado hajabahatika kutumia huduma za benki hiyo watapata
fursa ya kuuliza masuala mbalimbali kuhusu huduma zinazotolewa na Benki.
“Tumejipanga
vizuri, tunayo timu nzuri yenye uzoefu na masuala ya Kibenki
,watafafanua mambo mbalimbali kuhusu huduma za Amana benki kuanzia
masuala ya akaunti,miamala ya kimtandao na huduma zinazotolewa na
mawakala wetu kote nchini.Alisema Msabaha.
Ameongeza
kusema Kituo hicho kitafanya kazi siku saba katika wiki,pamoja na siku
za siku kuu jambo ambalo wanaamini litasaidia kufafanua mambo mbalimbali
yanayowahusu wateja.
“Namba
yetu ya huduma kwa mteja ni 0657 980 000, kupitia namba hiyo ni
matarajio yetu kuwa wateja watafurahia zaidi huduma tuliyoizindua kwani
ni rafiki kwa kila mmoja, imeandaliwa mahususi kabisa kuwapa uwezo
wananchi kupiga simu,kutuma ujumbe mfupi pamoja na njia zingine za
mitandao ya kijamii”.Alisema Msabaha
Kwa
mujibu wa Bw Msabaha kituo hicho kinatarajiwa kuleta mabadiliko kwenye
biashara kupitia huduma za kibenki huku akiongeza: “Ni adhma yetu
kuhakikisha kwamba tunapambana siku zote ili tu hali ya kiuchumi kwa
wateja wetu iendelee kuwa bora na ni hicho tu ndio kimekuwa kikitusaidia
kuwa na matokeo mazuri
Alibainisha
kuwa huduma hiyo ilibuniwa mahususi ili kuleta tija kwa wateja wa benki
hiyo kwa kuwa inaenda sambamba na mahitaji yao, mfumo wao wa maisha
pamoja na hadhi yao hatua aliyoilezea kuwa itaiongezea benki hiyo
uaminifu miongoni mwa wateja wake
Kwa
upande wake Mkuu wa idara ya Biashara ya Amana Benki Bw. Rajab Munir
amesema wateja wa Amana watapata fursa ya kuijua benki yao kwa undani
kwani sasa wanaweza kuulizwa maswali yao na kujibiwa kwa wakati ndani ya
masaa 15 katika wiki ikiwamo siku za siku kuu.
Alisema
hiyo ilikuwa dhamira yao ya muda mrefu na kuzinduliwa kwake imekuwa ni
faraja kwa wateja ambao sasa watafaidika nayo.kwa kupata majibu ya papo
kwa hapo kuhusiana na akaunti zao, miamala yao na misaada kuhusu kutumia
huduma za kimtandao.
katika
kipindi kisichopungua miaka mitano Tayari Benki ya Amana kwa
imefanikiwa kuwa na matawi saba matano yakiwa katika Jiji la Daresalaam
na mengine mawili yakiwa katika Jiji la Mwanza na Arusha.
Mipango
ya Baadae ni kwamba Amana benki inatarajia kufungua matawi mengine si
chini ya matatu kati ya Mkoa wa Tanga au Zanzibara kulingana na upembuzi
yakinifu utakaofanywa na benki hiyo |
No comments:
Post a Comment