Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sayansi) Prof. Simon Msanjila Akizungumza kwa Niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Wanataaluma ya Usimamizi wa Ardhi Kanda ya Afrika Mashariki jana jijini Dar es salaam. |
Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Prof. Idrissa Mshoro akizungumza na Mtandao wa
Wanataaluma wa Vyuo Vikuu Vinavyotoa Mafunzo yahusuyo Usimamizi wa Ardhi
Kanda ya Afrika Mashariki jana jijini Dar es salaam.
|
Washiriki
wa Mtandao wa Wanataaluma wa Vyuo Vikuu Vinavyotoa Mafunzo yahusuyo
Usimamizi wa Ardhi Kanda ya Afrika Mashariki kutoka nchi 9 za Bara la
Afrika wakifuatilia Mkutano wa mtandao huo jana jijini Dar es salaam. Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
Serikali
imewataka wataalam wa vyuo Vikuu vinavyotoa mafunzo ya Usimamizi wa
Ardhi waitumie taaluma yao katika kutafuta suluhisho la migogoro ya
Ardhi inayowakumba wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumza
kwa Niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi
wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Wanataaluma ya Usimamizi wa Ardhi Kanda
ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es salaam, Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo (Sayansi) Prof. Simon Msanjila amesema kuwa wataalam hao
wanalo jukumu la kufuatilia migogoro inayotokea nchini na kuhakikisha
wanatoa ushauri wa kitaalam utakaotoa majibu ya utatuzi wa migogoro
hiyo.
“Ninyi
kama watalaam wa sekta ya Ardhi lazima mtoe majibu kwa nini migogoro ya
ardhi inaendelea kutokea katika maeneo mbalimbali licha kuwepo kwa
kanuni, Sheria na taratibu zinazosimamia sekta ya Ardhi nchini” Amesema
Prof.Msanjila.
Ameeleza
kuwa wao kama watalaam wa sekta hiyo wanatakiwa kwenda zaidi kwenye
matatizo halisi na kuwawafikia wananchi wengi zaidi kwa kushirikiana na
wadau mbalimbali ili kuondoa changamoto zao kuliko kucheza na vitabu na
kuongea kwenye Ofisi.
Amewataka
wataalam hao hasa wale walioko nchini Tanzania kufika katika maeneo
yenye migogoro ya Ardhi ikiwemo Morogoro na maeneo mengine ili kuangalia
kwa nini wananchi wanaendelea na mapigano tunajua ipo migogoro ya Ardhi
inayotokea katika mikoa ya Morogoro, Pwani na mikoa mingine.
Amesema
kuwa kwa upande wa Serikali suala la ufumbuzi wa migogoro ya Ardhi
linaendelea kupewa kipaumbele kwa kuhakikisha kuwa ardhi inaendelea
kutolewa kwa kuzingatia sheria pia kushughulikia changamoto zote
zinazokwamisha ustawi wa sekta ya ardhi hususan uondoaji kero zote
zinazokwamisha matumizi bora ya ardhi kwa jamii.
Akifafanua
kuhusu nafasi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya
Ufundi katika mkutano huo ameeleza kwamba kupitia mkutano huo wa
kitaalam wa masuala ya Ardhi, Wizara hiyo inajifunza kuhusu changamoto
zitakazojitokeza na kuibuliwa ili ziwekwe kwenye mitaala kwa lengo la
kuwaandaa watalaam watakaokuwa na uwezo wa kusuluhisha matatizo yote
yanayojitokeza kwenye sekta hiyo.
Amesema
kuwa Sekta ya Elimu kupitia mkutano huo itaboreshwa kwa kupata nyongeza
ya utalaam kutoka kwa wataalam kutoka Vyuo vikuu vya nchi mbalimbali za
Bara la Afrika waliohudhuria mkutano huo na kuongeza kuwa Chuo Kikuu
Ardhi nchini Tanzania ambacho kimebobea kwenye masuala ya Ardhi kitapata
taarifa zaidi katika uboreshaji wa mitaala na mafunzo ya Programu za
Utawala wa Ardhi, Ugawaji wa Ardhi na Upimaji wa Ardhi”
Kwa
Upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Prof. Idrissa Mshoro
akizungumza mara baada katika mkutano huo amesema kuwa wataalam wa Ardhi
nchini Tanzania bado wana umuhimu mkubwa katika maendeleo ya sekta ya
Ardhi na kufafanua kuwa wao kama chuo kinachozalisha watalaam wa Ardhi
wanalo jukumu kuzalisha watalaam watakaofanya usimamizi thabiti wa Ardhi
kukabiliana na changamoto zilizopo.
“Sisi
nafasi yetu kama Chuo Kikuu Ardhi ni kujua ni namna gani tunavyoweza
kuzalisha wataalam wa kutosha wenye weledi watakaoweza kukabiliana na
changamoto mbalimbali zilizoko kwenye sekta ya Ardhi pia kuhakikisha
wataalam tunaozalisha wanakidhi ubora na matarajio ya wananchi” Amesema
Prof. Mshoro.
Amesema
kuwa wanataaluma kutoka Tanzania watanufaika kutokana na mkutano huo kwa
kuwa unawajumuisha watalaam wa Ardhi kutoka takribani nchi 9
watakaobadilishana uzoefu kuhusu changamoto mbalimbali za ardhi
zinazojitokeza katika maeneo yao na namna wanavyozitatua.
Aidha,
amesema kuwa Sekta ya Ardhi nchini Tanzania bado inakabiliwa na uhaba wa
watalaam wa kutosha ambao wangeweza kusimamia maamuzi katika masuala
ya Ardhi ngazi za chini na kuongeza kuwa ili kupata maamuzi na taarifa
sahihi za ardhi ni lazima suala la uwepo wa watalaam hao liendelee
kupewa kipaumbele.
Kuhusu
mchango wa watalaam hao katika utatuzi wa migogoro ya Ardhi amesema kuwa
ipo haja ya watalaam waliopo kutumika ipasavyo kutatua migogoro
inayojitokeza na kuwaletea manufaa wananchi ambao wanahitaji huduma za
wataalam hao.
Mkutano huo unaohusisha Mtandao wa vyuo Vikuu Huo ni mkutano wa nane nane wa mwake
Amesema
kuwa tayari kwa upande wa Serikali tayari watalaam wa sekta husika
wamejipanga kuhakikisha kuwa wanapata suluhisho la mgogoro inayojitokeza
kupitia sheria zilizopo |
No comments:
Post a Comment