Wajumbe wa bodi na waandishi habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Spika Mstaafu, Anne Makinda.
( picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii’)
………………………………………………………………………………
Na Chalila Kibbuda, Globu ya Jamii.
BODI
ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) imefanya maboresho kwa
kupunguza idadi ya wakurugenzi kutoka tisa hadi watano ili kuweza
kufanya kazi kwa kasi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Akizungumza
na waandishi habari Makao Makuu NHIF leo Mwenyekiti bodi hiyo Spika
Mstaafu, Anne Makinda amesema kuwa utaratibu wa awali wakurugenzi
walikuwa wanaajiliwa kwa mikataba ya miaka mitatu mitatu.
Amesema
kuwa wakurugenzi waliokuwa wanafanya wengine kwa mikataba wengine
wamemaliza na ambao walikuwa wanaendelea wamesitisha mikataba yao.
Makinda amesema kuwa NHIF imekaa kwa muda ikiwa haina bodi kwa mwaka mmoja na nusu hivyo baadhi ya vitu havikuwa sawa.
Amesema
kuwa watu ambao wamemaliza mikataba na weengine kusitisha mikataba yao
wanaweza wakaomba tena kama wana sifa ya kazi watazoomba na kuangalia
weledi wao
|
No comments:
Post a Comment