Na Anitha Jonas – MAELEZO, MBULU
…………………………………………………
Uongozi
wa Wilaya ya Mbulu watakiwa kufuatilia Mikataba ya wanariadha wa nao
chukuliwa na vya watu binafsi kwa ajili ya kuwapeleka katika mashindano
ya Kimataifa
Kauli
hiyo imetolewa leo Mjini Mbulu na Naibu Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura alipofanya ziara
ya kikazi wilayani hapo kukutana na wanariadha kujadili changamoto zao
na kupata ushauri wa nini kifanyike kuboresha michezo hiyo.
“Ninataka
kuona wanariadha wa kitanzania wanafanikiwa na kkuwa na maendeleo ya
kiuchumi illikuona faida ya kufanya mchezo huo pamoja na kuwapa
motisha vijana wadogo kuipenda riadha msiwe ni watu wa kubaki na medali
tu bila kuonyesha faida mliyopata kutokana na Medali hiyo”,alisema
Mhe.Wambura.
Naibu
Waziri Wambura aliendelea kusema Wilaya ya Mbulu imejaliwa kuwa na
vipaji vya kipekee katika riadha na serikali imejipanga kuhakikisha
wanariadha nchini wanapata kuwa na maendeleo ya kiuchumi na kufanya
watu heshimu michezo hiyo na kuona thamani yake kama ilivyo kwa nchi za
nje.
Kwa
upande wa Mwaanariadha wa zamani aliyena sifa kubwa katika rekodi za
Dunia Mzee John Stephen Akhwari alisema Mchezo wa riadha umekuwa
ukiletea sifa nchi lakini umeingiliwa na changamoto ya watu hao
wanaochukua vijana na kuwapeleka nje ambapo katika Mashindano na
wanaposhinda kuwaibia pasibo wao kujua kutokana na uelewa mdogo wa
masuala ya kiuchumi.
Akiendelea
kuzungumza Bw.Akhwari aliiomba serikali kutafuta wadau watakao jenga
uwanja wa michezo wilayani hapo pamoja kwa ajili ya kukuza vipaji hivyo
vya riadha vilivyoko wilayani hapo na sababu kubwa ya kujenga uwanja huo
katika eneo hilo ni hali ya hewa ya ubaridi ni nzuri kwa mchezo huo.
Pamoja
na hayo naye Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Bw.Chelestino Mofuga alisema wako
tayari kuhakikisha wapo tayari wanariadha hao wanapata faida kutokana
ushindi wanaoupata katika mashindano mbalimbali wanayoshiriki.
Hata
hivyo wanamichezo hao wa mbulu wamepewa angalizo la kutojaribu kutumia
madawa ya kuongeza nguvu katika michezo kwani ni kinyume na maadili ya
michezo.
No comments:
Post a Comment