VIONGOZI na Watendaji wa CCM Zanzibar wametakiwa kuendelea kuwa
wabunifu katika kuimarisha miradi ya maendeleo ya Chama hicho ili iwe
ya kisasa na inayoendana na mazingira ya sasa kiuchumi.
wabunifu katika kuimarisha miradi ya maendeleo ya Chama hicho ili iwe
ya kisasa na inayoendana na mazingira ya sasa kiuchumi.
Kimesema miradi hiyo inatakiwa kuimarishwa kwa lengo la kufikia hadhi
na thamani ya CCM, hatua itakayotoa fursa ya mapato yanayotokana na
rasilimali hizo kuwanufaisha wanachama wengi badala ya watu wachache.
Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vua
katika mwendelezo wa ziara yake ya kuhakiki na kukagua mali za chama
huko katika Mkoa wa Mjini Kichama Unguja.
Alisema ubunifu ndiyo nyenzo pekee ya kuongeza thamani ya miradi
inayoanzishwa kwani itakuwa na miundombinu ya kisasa inayokubalika
katika ushindani wa kibiashara.
Alieleza kwamba miradi mbali mbali iliyopo hivi sasa haipo katika
mazingira mazuri ya kibiashara hali inayopelekea kupatikana kwa mapato
kidogo, chanamoto inayotakiwa kufanyiwa kazi na wahusika kiutendaji.
“Naamini kwamba kama tutatumia rasilimali zetu vizuri kujiimarisha
kiuchumi tunaweza kupiga hatua kubwa kiuchumi, kwani maeneo yetu kwa
mfana kama tutajenga maduka na kumbi za mikutano za kisasa tunaweza
kupata mapato mengi tofauti na yanayopatikana hivi sasa., alisema
Vuai.
Vuai alifafanua kwamba Rasilimali na Miradi ya chama hicho imetokana
na nguvu za waasisi na wazee wa Afro Shiraz Party( A.S.P) kabla ya
kuzaliwa CCM walionunua rasilimali za kudumu ambazo kwa sasa
zinawanufaisha vizazi vya sasa, hivyo na viongozi na watendaji waliopo
sasa kwa ngazi mbali mbali ndani ya chama hicho wanatakiwa kuiga mfano
huo.
Alisema CCM ni taasisi ya kisiasa lakini bado inatakiwa kuendelea kuwa
na falsafa ya kufanya siasa na uchumi kama sera za chama hicho
zinavyoelekeza, hivyo wahusika wanatakiwa kuwa na mipango mizuri ya
uendeshaji wa miradi ya chama ili kuepuka marumbano yasiyokuwa ya
lazima ndani ya chama hicho.
“ Kwanza nakupongezeni kwa kuona umuhimu wa kuanzisha miradi lakini
tunahitaji kufahamu kwamba suala la kuanzisha ni jambo moja lakini
kuienzi na kuiendeleza ni mambo mengine na ya msingi yanayotakiwa
kupewa kipaumbele.
Pia katika kuimarisha miradi hii ni lazima tuzingatie suala la uwazi
hasa kupeana taarifa sahihi za vyanzo vya mapato na mipango mingine ya
maendeleo kupitia vikao halali vya kikanuni ili Wana CCM na viongozi
wengine wapate taarifa hatua itakayoepusha malalamikoi na shutuma
zisizokuwa za lazima.”., alishauri Vuai na kuongeza kuwa miradi
inayohusu fedha inahitaji uwazi na udilifu wa hali ya juu katika
uendeshaji wake kwani inagusa maslahi ya umma nasi mtu mmoja.
Alieleza kwamba lengo la ziara hiyo ni kukagua miradi na mbali mbali
za chama ili kubaini changamoto zilizopo katika rasilimali hizo na
kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu kwa maendeleo ya CCM.
Alisema toka ameanza kufanya ziara hiyo kuna baadhi ya maeneo amebaini
kujitokeza kwa vitendo vya udanganyifu na utapeli vinavyofanywa na
baadhi ya watu wasiowaaminifu wanaohujumu mali za chama hicho kwa
makusudi hali ambayo CCM haiwezi kuvumilia na itachukua hatua stahiki
dhidi yao.
Naibu Katibu Mkuu huyo, aliendelea kusisitiza viongozi wote
wanaoendesha miradi ya chama kujiridhisha juu ya mikataba wanayofunga
na wawekezaji ama wafanyabiashara, kuhakikisha inaenda sambamba na
sera ya uchumi inayoelekeza miradi yote mikubwa kusimamiwa na Baraza
la Wadhamini la Chama hicho.
Aliongeza kwamba CCM Afisi Kuu Zanzibar ipo tayari kutoa ushauri wa
kisheria juu ya umiliki na uendeshaji wa miradi mbali mbali ya Chama
kwa nia ya kuziweka mali za CCM katika mazingira salama.
Aidha Vuai aliahidi kuhakikisha Changamoto, maoni na ushauri
vilivyojitokeza katika ziara hiyo atahakikisha Afisi yake wanazifanyia
kazi kwa haraka ili sehemu husika waweze kupata mrejesho utakaosaidia
kusonga mbele kimaendeleo kama utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM
ya mwaka 2015/ 2020 unavyoelekeza.
Nao viongozi wa maeneo yaliyofasnyiwa ziara katika Mkoa huo,
wamepongeza hatua ya CCM kukagua miradi yao na kuahidi kuyafanyia kazi
kwa vitendo ushauri na maagizo yote yaliyotolewa na chama hicho.
No comments:
Post a Comment