Na Daudi Manongi,MAELEZO
Wakala wa Vipimo Tanzania
imewafungulia kesi mahakamani wafanyabiashara saba waliokuwa wakifanya
uchakachuaji wa mizani za kupimia Pamba ambapo kati ya kesi hizo nne
zimetolewa hukumu na wafanyabiashara hao wamelipa faini na zilizobakia
ziko mahakamani.
Hayo yamesemwa na Kaimu Meneja wa Elimu, Habari na Mawasiliano wa Wakala wa Vipimo (WMA), Irene John alipokuwa
akieleza hatua zilizochukuliwa hadi sasa baada ya kuwepo kwa
malalamiko mengi kutoka kwa wakulima wa pamba hususani kanda ya ziwa.
Bi.Irene amesema kuwa kila
ukifika msimu wa pamba wanunuzi hao hutumia mizani iliyochakachuliwa na
kuwaibia wakulima na hivyo msimu huu ulivyoanza wakatuma maofisa wao
katika vituo vyote vinavyonunua pamba ili kuhakikisha uuzaji wa pamba
unafanyika kwa kutumia vipimo sahihi kwa lengo la kumlinda mkulima na
katika ukaguzi huo wamefanikiwa kukamata wafanyabiashara hao wasio
waaminifu.
Aidha amesema kuwa kabla ya
kutuma wataalamu wake, wakala wa vipimo(WMA) ilituma wataalaumu wake
kuzunguka mikoa yote inayolima pamba hususani Kanda ya Ziwa ili kutoa
elimu kwa wakulima na wafanyabiashara kuacha udanganyifu huo kwani
unaathiri sekta nzima ya kilimo hicho.
Aliongeza kuwa uchakachuaji huu
umeifanya pamba ya Tanzania kila inapofika katika soko la dunia
kushushwa bei kwa kukosa ubora ukilinganisha na zamani ambapo pamba ya
Tanzania iliitwa dhahabu nyeupe kwenye soko la dunia na kuchukua alama
ya kwanza kwa ubora wa pamba yetu, hivi sasa hali imebadilika baada ya
kuzuka mchezo huo michafu.
Kaimu Meneja uyo wa Elimu,Habari
na Mawasiliano amewaasa pia wakulima kuacha mtindo wa kuweka maji,
mchanga na hata mawe ili kupata kilo nyingi katika pamba kwani
vinaathiri mbegu na hivyo kupotea thamani ya zao lenyewe na kuhaidi
zoezi hili la ukaguzi litaendelea mpaka msimu wa pamba utakapoisha mwezi
wa nane.
Aidha amesema kuanzia mwaka huu
adhabu ya uchakachuaji wa mzani wa kupimia pamba ni faini ya shilingi
elfu 50 au miaka mitatu jela.
|
July 15, 2016
WAFANYABIASHARA 7 MBARONI KWA UCHAKACHUAJI WA MIZANI ZA KUPIMIA PAMBA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment