Agizo
la Jeshi la Polisi nchini la kusitisha kufanyika kwa mikutano ya
hadhara ya kisiasa imeonekana kutoathiri ratiba za Mbunge wa Bariadi,
John Chenge ambaye ameendelea na mikutano ya hadhara jimboni kwake.
Taarifa
kutoka jimboni humo zimeeleza kuwa Chenge amekuwa akifanya mikutano ya
hadhara katika vijiji mbalimbali na Alhamisi iliyopita alianza na eneo
la Buchani, mkutano uliomalizika salama bila kuwepo kizuizi chochote.
Katika
mikutano hiyo, Mtemi Chenge ameendelea kuwasisitiza wananchi wake
kupuuza kauli za kisiasa zinazotolewa na wapinzani wake bali waangalie
namna anavyotekeleza ahadi alizozitoa kwenye kampeni za uchaguzi mkuu.
Mikutano hiyo ya Chenge hutanguliwa na matangazo yanayofanywa kwa kutumia magari yenye vipaza sauti katika eneo husika.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Onesmo Lyanga alipotafutwa kwa njia ya simu
alisema kuwa yeye hahusiki kutoa vibali vya mikutano na kwamba mhusika
ni Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD). Hata hivyo, OCD hakupatikana kwa wakati.
Hali
hiyo imedaiwa kuzua manung’uniko kwa vyama vya upinzani mkoani humo
ambavyo vimeshindwa kufanya mikutano ya hadhara kutokana na kuwepo kwa
zuio la Mikutano hiyo nchi nzima.
Mwezi
uliopita, Kamishna wa Jeshi la Polisi, Operesheni ya Mafunzo, Nsato
Msanzya alitangaza kupiga marufuku kufanyika kwa mikutano ya kisiasa kwa
sababu za kiusalama.
“Polisi
kupitia vyanzo vyake mbalimbali, imebaini kuwea mikutano hiyo ina lengo
la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi,” alisema Kamishna Nsato.
Kufuatia
agizo hilo, Jeshi la Polisi lilizuia kufanyika kwa mikutano iliyokuwa
imepangwa na Chadema na ACT-Wazalendo kwa nyakati tofauti.
|
July 18, 2016
CHENGE AKAIDI AGIZO LA JESHI LA POLISI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment