Siku
chache baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kutoa agizo
la msako wa nyumba hadi nyumba ili kuwabaini watu wasio na kazi maalum,
Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita aliibuka na kudai agizo hilo
ni batili na haliwezi kutekelezeka kwa mujibu wa sheria, kanuni na
taratibu za nchi.
Jukwaa
Huru la Wazalendo kwa Mkoa wa Dar es Salaam kupitia kwa Mwenyekiti wake
Andrew Kadege wamelaani vikali kitendo kilichofanywa na Meya wa Dar es
Salaam, Isaya Mwita kwa kufanya harakati za siasa badala ya zile za
kuwaletea wananchi maendeleo huku akiwapotosha kwa makusudi wananchi na
kuwataka kukaidi agizo la Makonda.
Jukwaa
Huru la Wazalendo Tanzania limewataka wananchi wa Dar es Salaam na
Tanzania kwa ujumla kutoa ushirikiano mara zoezi la kuwatambua wakazi
katika kaya litakapoanza rasmi ili kupata takwimu sahihi kwa maendeleo
ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla hususan katika kipindi hiki
ambapo serikali inataka kuanza ugawaji wa Sh. Milioni 50 kusaidia
maendeleo ya kaya.
Hata
hivyo jukwaa limemtaka meya kutokuendelea na tabia ya kuwalaghai
wanainchi kutoshiriki katika shughuli za maendeleo kwani ndio sehemu yao
ya kujikwamua kiuchumi na kuondoa umasikini unaowakabili watanzania
kwa ujumla.
Jukwaa
limeongeza kuwa hatua hiyo ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ya
kutaka kuwatambua wanainchi wa mkoa wake wa Dar es salaam katika
ngazi ya kaya ni kutaka kujua jinsi gani ya kuweza kupanga na
kuwahudumia kama ilivyo katika majiji ya London,Paris na Berlin
inavyofanyika.
Jukwaa
huru limechukua nafasi hiyo kuwaomba na kuwashauri wanainchi wote
popote litakapo fanyika zoezi hilo kushirikiana na serikali kikamilifu
kwani ni kwa manufaa ya wanainchi wenyewe na taifa kwa ujumla ili
kuweza kuinua uchumi.
|
July 18, 2016
JUKWAA HURU LA WAZALENDO LALAANI MAAMUZI YA MEYA WA DAR ES SALAAM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment