SEREKALI
imemtaka Dk Mwaka kwenda kwenye sheria kama hajaridhika na uamuzi wa
serikali wa kukifungia kituo chake cha tiba za asili.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia,wazee na
watoto Ummy Mwalimu wakati akiongea na wadau wa afya katika hospital ya
Rufaa ya Mkoa wa Kagera.
Ummy
alisema kuwa uamuzi uliofanywa na serekali wa kukifunga kituo cha afya
cha dk Mwaka ni sahihi kwani hajaonewa kwasababu matangazo na huduma
alizokuwa akitoa zilikuwa haziendani na maadili na taratibu za udaktari.
"Dk
Mwaka asichonganishe wananchi na serekali yao kwamba tumewafungia
huduma walizokuwa wakipata kwake wakati huduma alizokuwa akitoa hazikuwa
na sifa"alisema Ummy
Alisema kuwa kama anaona ameonewa aende mahakamani ili sheria ifuate mkondo wake."Kama anaona tumemuonea aende mahakamani tutakutana huko"alisema
No comments:
Post a Comment