KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

July 26, 2016

JK:NASHUKURU MUNGU KWANI NIMEACHA NCHI SALAMA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEimsLbwDU2rNjF7oAKIp6oi4Vo2SKbj9AoDB0mk8Bphp32XK93yUjJTVF2CSM9dvU_bZGZSidXDy6eIldVMKfK_7tIM2Qfl4v_T5sWDqdI6A6YXqyjcITqsdsarTZlFFjnI9iYkt8W7iyY/s1600/4.JPG
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akisalimiana na Mke wa Rais  Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete,mama Salma Kikwete, katika hafla ya  kumkaribisha nyumbani mwenyekiti huyo mstaafu wa CCM,iliyofanyika
wilayani Bagamoyo,wengine ni wabunge wa mkoa huo wakimsalimia Mwenyekiti huyo mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjcxYKOFsipkJr9JcMfjVcb50go1k342luoq8-N1x49WEzAPiitTPxPokv2HYqoooKbiR6LjvPOANxaI-xK_TqhRDFEeUxQK1u2qsclx1Qrh8ln3jXf6B9jqOoqsJx9Nj4eXwAW7vLeS1A/s1600/1.JPG
Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.Jakaya Kikwete akizungumza na wananchi na wafuasi wa Chama cha Mapiduzi katika hafla ya kumkaribisha nyumbani mwenyekiti huyo mstaafu wa CCM,iliyofanyika
wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Na David John Pwani


MWENYEKITI Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.Jakaya Kikwete amesema anashukuru Mungu Kwa kuutua mzigo salama huku akiicha nchi  ikiwa salama tulii kabisa.

Amesema kuwa safari yake ya urais ilianzia Bagamoyo akitokea wilayani hapo ambapo baada ya hapo alikwenda Kibaha kutangaza nia ya kugombea urasi nakudai kuwa amejisikia flaha kurudi tena Bagamoyo akiwa salama.

Amesema wakati akielekea kutanga nia ya kugombea urais alikuwa na mtoto wake Ridhiwani Kikwete ambapo yeye alikuwa anaandika na Ridhiwani anachapa kwenye Komputa.

Dkt.Kikwete ameyasema hayo leo wilayani Bagamoyo katika hafla ya kumkaribisha Nyumbani baada ya kuitumikia nchi Kwa miaka mingi, ambapo iliandaliwa na Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani.

Alisema.anashukuru Kwa Mara nyingine kurudi mahala alipoazia na kwamba amemaliza salama na ameacha nchi ikiwa salama na imetulia tulii kama Maji kwenye mtungi. Akikumbuka mchakato wa mwakajana wa kumpata Mgombea ulikuwa na mambo mengi lakini mambo yalikwenda salama na hakuna lililokuwa limeharibika .


"Ilikuwa Kazi kubwa si ndogo lakini hatimaye wa kavuka na wakaingia kwenye uchaguzi ambao ulikuwa na vurumayi"amesema Dkt.Kikwete .Aidha amesema kuwa hata hivyo katika uchaguzi huo kulikuwa hakuna mtu ambaye alipatwa na tukio la kumpiga mwezake hali ambayo iliwashangaza hata nchi jirani.

Alisema kuwa katika kipindi chake cha uongozi amefanya kazi kubwa ya kusukuma maendeleo ya wananchi Kwa mikoa yote,wilaya zote bila ubaguzi wowote ule huku akikiri kukabiliana na Changamoto ya kunyoshewa vidole hususani pale alipojalibu kupeleka maendeleo Wilayani Bagamoyo konakamba wananchi wa Bagamoyo walikuwa
hawana haki.

Aidha Dkt.Kikwete alisema kuna wakati alisimamisha  fedha za ujenzi wa barabara hiyo na kupeleka fedha hizo kujenga barabara ya Geita, Sengerema,usagala ,na kulizuka na Maneno mengi dhidi yake na hadi kufikia wabunge kulumbana.

Amesema hata hivyo anashukuru kwamba amemaliza salama na Kwa Bahati nzuri amepatikana rais ambaye ana ari kubwa ya kuwaletea maendelea watu huku akitaka watanzania kumuunga mkono.
Wanachana

Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani leo wamejitokeza Kwa wingi kumkaribisha nyumbani Mwenyekiti Mstaafu wa Chama hicho Dkt.Jakaya Kikwete katika sherehe zilizofanyika wilayani Bagamoyo. Wanachama hao ambao walitoka katika wilaya zote za Mkoa wa Pwani wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho mkoa Masikuzi. pamoja na Katibu Joyce Masunga walimuaga na kumkaribisha
Kwa nyimbo mbalimbali.

No comments:

Post a Comment