Dar es Salaam,
Kampuni
ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania leo imetangaza kubadilisha huduma
yake ya fedha ya M-Pesa kutoka teknolojia ya awali ya G1 kwenda mpya ya
G2, lengo kubwa ikiwa ni kuboresha
huduma hii kwa kuiingiza katika teknolojia ya juu ili iweze kupatikana
wakati wowote kwa uhakika na kwa kasi kubwa wakati wa ufanyaji wa
mihamala ya malipo na huduma mbalimbali.
Matumizi
ya teknolojia mpya ya G2 ambayo miundombinu yake imejengwa hapa nchini
itarahisisha matengenezo yake pindi yatakapojitokeza matatizo
ya kimtandao pia itawezesha kupanuka kwa matumizi ya huduma hii kwenye
kuboresha na kuunganisha huduma mbalimbali na kibiashara.
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa matumizi ya teknolojia hii mpya katika hafla
iliofanyika leo,Afisa Mtendaji Mkuu wa huduma za malipo ya mtandao
wa Vodacom Tanzania, Sitoyo Lopokoiyit amesema “Tunawaletea huduma
ya M-pesa katika teknolojia mpya na bora zaidi,tunajivunia kwa kazi
nzuri iliyofanyika kufanikisha mabadiliko haya ambayo yatawawezesha
watanzania kupata huduma bora za kifedha kupitia
huduma ya M-Pesa iliyoboreshwa zaidi.Ubunifu na matumizi ya teknolojia
hii mpya yataboresha huduma hii sio kwa wateja wa Vodacom pekee bali
biashara mbalimbali na huduma zinazofanyika kupitia huduma hii”
Sitoyo
aliongeza kusema kuwa teknolojia hii italeta mapinduzi makubwa ya
matumizi ya huduma za kifedha kwa njia ya mtandao wa simu na Vodacom
itaendelea kujenga mazingira ya kukuza biashara za malipo kwa njia ya
mitandao na kuzidi kuiweka Tanzania mbele katika huduma za biashara kwa
njia ya mtandao pia kuongeza wigo wa huduma za kimtandao kama vile
kuweka akiba,kuchukua na kulipa mikopo,ufanyaji
wa mihamala ya malipo kwa mtandao,huduma za bima na huduma nyinginezo
nyingi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Huawei,Bruce Yang alisema “Kupitia
teknolojia ya kiwango cha juu ya Huawei,Huduma za M-Pesa zimebadilika
kabisa na kuwa za kiwango kikubwa cha ubora na imeboreshwa zaidi kuweza
kukidhi matakwa ya huduma mbalimbali za kifedha.Kwa kutumia timu ya
wataalamu wetu tumeweza kujenga miundombinu ya kisasa itakayowawezesha
watanzania kupata huduma za kifedha kwa viwango
vya kimataifa.Tumefurahishwa na ushirikiano tulioupata kutoka timu
nzima ya wafanyakazi wa Vodacom hali iliyotuwezesha kumaliza mradi huu
wa kubadilisha teknolojia mapema tofauti na jinsi tulivyotegemea”
Huduma
ya M-Pesa ya Vodacom Tanzania ikiwa ni ya kwanza kwa kutuma , kupokea
fedha na kufanya mihamala mbalimbali ya malipo inaaminika kwa watanzania
wengi.Tangia ianzishwe katika kipindi cha miaka 8 iliyopita inao
watumiaji wapatao milioni 9.Kupitia teknolojia hii mpya ya G2,huduma za
M-Pesa zimeboreshwa kuwa nzuri na ubunifu wa kutumiwa kwa malipo,
huduma mbalimbali na kuwa na uwezo wa kuunganisha biashara
.Mabadiliko haya ni ya kihistoria katika huduma za kifedha kwa njia ya
simu nchini Tanzania na kampuni inawahaidi watumiaji wategemee ubunifu
wa kila aina kwa matumizi ya huduma hii katika teknolojia hii ambayo
kuanza kwake kutumika nchini ni mafanikio makubwa
katika kuboresha huduma za kifedha kwa watanzania . Vodacom Tanzania
inajivunia kufanikisha kuleta teknolojia hii ambayo inategemewa kuleta
mapinduzi makubwa ya huduma za kifedha nchini.
No comments:
Post a Comment