WAZIRI
MKUU Kasim Majaliwa amesema Serikali itahakikisha inaunga mkono dini
zote nchini na kuzipa ushirikiano wa kutosha ili ziweze kufanya kazi
zake vizuri.
“Dini
ndiyo inayojenga msingi imara kiroho, kiimani na ndiyo inajenga maadili
mema. Leo tunaposema kila mtu awe muadilifu tumegundua ili tufanikiwe
lazima tuweke mazingira mazuri yatakayowezesha madhehebu yote kuabudu
kwa uhuru,” alisema.
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo jana (Alhamisi Julai 14, 2016) wakati
akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Malolo na
Chimbila ‘B’ akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu ya
kukagua shughuli za maendeleo wilayani Ruangwa.
Alisema
Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk. John Magufuli imegundua
kuwa ili iweze kufanikiwa ni lazima ishirikian na madhehebu ya yote ili
yaweze kufanya kazi zake vizuri.
“Nikiwa
mtendaji mkuu wa shughuli za Serikali niliamua kuunda kamati ya amani
ya Taifa ambayo inajumuisha viongozi wa dini zote. Pia nimeiagiza mikoa
na wilaya zote kuunda kamati za amani ili kuhakikisha umoja na maelewano
miongoni mwa dini zote nchini unakuwepo,” alisema.
Alisema
lengo la kamati hizo za amani ni kuhakikisha Watanzania wote wanakuwa
na maadili mema na kutambua umuhimu wa kuimarisha amani na utulivu
nchini.
Akizungumzia
tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika vijiji
vya Nanganga, Nangumbu, Mbecha, Malolo, Mpumbe na Chimbila ‘B’ alisema
Serikali inalifanyia kazi suala hilo.
Alisema
tayari mtaalamu wa kufanya utafiti wa maji chini ya ardhi ameshawasili
katika wilaya hiyo na baada ya kukamilisha utafiti huo shughuli ya
uchimbaji visima itaanza.
Waziri
Mkuu alisema lengo la utafiti huo ni kutaka kubaini wingi na ubora wa
maji katika eneo husika hivyo aliwataka wananchi wa eneo hilo kuwa na
subira wakati suala hilo likishughulikiwa.
|
July 15, 2016
MAJALIWA:SERIKALI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA MADHEHEBU YOTE NCHINI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment