Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Lekujan Manase (wa kwanza kushoto) akioneshwa moja ya mtambo wa kuendeshea kivuko (propulsion unit) alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko kipya cha Mv Pangani unaofanyika katika eneo la Bandari ya Dar es Salaam. |
Kivuko kipya cha Mv Pangani katika hatua za kukamilika kwa ujenzi wake, unaofanyika katika eneo la Bandari ya Dar es salaam.
Picha na Theresia Mwami,TEMESA
……………………………………………………………………………..
Na Theresia Mwami – TEMESA
Ujenzi
wa kivuko kipya cha Mv Pangani uko katika hatua za mwisho na
kinategemea kumamilika Julai mwaka huu na kuanza kutoa huduma.
Hayo
yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA)
Mhandisi. Lekujan Manase alipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa
kivuko hicho ambao upo mbioni kukamilika kwa kuanza kutoa huduma kwa
wananchi.
“Kivuko
hiki kipo katika hatua za mwisho za ujenzi wake na leo tumekuja hapa
kukagua mitambo ya kuendeshea kivuko (propulsion units) pamoja na injini
zilizofungwa katika kivuko hiki ili kukamilisha ujenzi wake na hatimaye
kianze kufanya kazi” alisema Mhandisi Manase.
Kwa
upande wake Mkurugenzi kutoka Idara ya Huduma za Ufundi na Umeme kutoka
Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Dkt. William Nshama
alieleza kuwa ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa kivuko hicho unaofanywa
kwa kiwango cha kimataifa na kuwa kivuko cha Mv Pangani kinatarajiwa
kutoa huduma kati ya Pangani na Bweni Mkoani Tanga baada ya ujenzi wake
kukamilika.
Kwa
mujibu wa kampuni ya Songoro Marine Transport LTD kivuko hicho kina
uwezo wa kubeba magari sita na abiria 100 kwa pamoja, na ni sawa na
uzito wa tani 50.
|
No comments:
Post a Comment