Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
Mkuu
wa wilaya ya Bagamoyo Majid Hemed Mwanga, amerudisha heka 900 kwa
wananchi, zilizokuwa zinamilikiwa na wawekezaji bila ya kufuata sheria
ya umiliki Ardhi, katika kijiji cha Pongwe Msungura kata ya Msata.
Uamuzi huo aliutangaza katika mkutano wa hadhara ulioitishwa kijijini hapo ili kujadili kero mbalimbali za wananchi.
Kati
ya keri zlizojadiliwa ni pamoja na tuhuma za ubadhilifu wa fedha kwa
viongozi wa Halmashauri ya kijiji hicho na kufanya maamuzi ya kugawa
Ardhi bila ya kufikisha taarifa kwenyemkutanomkuu wa kijiji.
Majid alisema wawekezaji hao wawili ambao kila mmoja anadai kumiliki
heka 500 hali ya kuwa taratibu za kisheria hazijafutwa, huku wananchi
wa kijiji cha Pongwe Msungura ambao ndio wajumbe wa mkutano mkuu wa
kijiji,walithibitisha kupitisha umiliki wa heka 50 peke.
Wananchi hao walisema hawatambui umiliki wa heka 500 kila mmoja kwa wawekezaji hao.
Kufuatia
hali hiyo Mkuu wa wilaya aliwataka wawekezaji hao kutoa maelezo namna
walivyopata maeneo hayo ambapo walionyesha mihutasari ya kijiji ambayo
imewapitishia kumiliki heka 500 kila mmoja.
Ili kujiridhisha na mihutasari
hiyo, mkuu wa wilaya alilazimika kusoma muhutasari wa tarehe 08 julai
2013 unaodaiwa kuandaliwa na mkutano wa kijiji ili kupitisha heka 500
kwa muwekezaji.
Alitaja jina moja baada jingine ambapo wananchi wote waliukataa muhutasari huo kwamba hawaujui.
Baada
ya hali hiyo, mkuu wa wilaya aliamuru kila muwekezaji kurudisha heka
450 na kubaki na 50 kama walivyopitishiwa na mkutano wa kijiji na hivyo kufanikiwa kurudisha heka 900 kwa wananchi.
Baada
ya kasoro mbalimbali zilizobainika katika mkutano huo, wajumbe wa
Halmashauri ya kijiji walipiga kura ya kumuondoa mwenyekiti wa kijiji
hicho Mbaraka Rajabu Mwelekwa.
Hata hivyo baada ya siku 90 mkurugenzi ataitisha mkutano utakaomchagua mwenyekit mpya wakijiji cha Pongwe Msungura .
|
July 19, 2016
MKUU WA WILAYA YA BAGAMOYO AREJESHA HEKARI 900 KUTOKA KWA WAWEKEZAJI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment