Na. Immaculate Makilika- MAELEZO, Dodoma
…………………………………
Mstahiki
Meya wa mji wa Dodoma Jaffari Mwanyemba, amesema kuwa watanzania
wanatakiwa kuwaenzi Mashujaa waliopigana katika vita mbalimbali ikiwa
ni katika harakati za kuiletea uhuru nchi ya Tanzania.
Hayo
yamesemwa leo saa sita usiku, wakati alipokuwa akizima Mwenge wa uhuru
uliowashwa jana Julai 24, na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini
Mheshimiwa Christina Mndeme katika kilele cha mnara wa mashujaa mnano
saa 6 kamili usiku ikiwa ni sehemu ya maombolezo ya kumbukumbu ya
Mashujaa, yaliyofanyika katika Uwanja wa Mashujaa uliopo mjini Dodoma.
“Watanzania
tuna jukumu la kuwaenzi Mashujaa kwa kufanyakazi kwa bidii, nidhamu na
uadilifu, na kama wote tutafanya hivyo tutakuwa tumewaenzi mashujaa
wetu” alisema Mstahiki Meya Mwanyemba
Ameongeza
kuwa kila mwananchi atimize uwajibu wake kwa kufanyakazi, ili kila
mmoja atapata haki yake na hivyo kuendelea kudumisha amani iliyopo
nchini.
Maadhimisho
ya kumbukumbu za Mashujaa kwa mwaka huu yamefanyika leo julai 25,
mkoani Dodoma ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Magufuli alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo.
No comments:
Post a Comment