Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt.Rufaro Chatora akiongea na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu wakati alipoenda kumuaga rasmi ofisini kwake.Dkt.Chatora amemaliza muda wake wa kufanya kazi nchini Tanzania na hivyo kuhamishiwa nchini Afrika ya Kusini. |
Waziri
Ummy Mwalimu akifanya mazungumzo na mwakilishi huyo,Dkt.Chatora
amesisitiza wizara kujenga uwezo wa ndani katika kukabiliana na magonjwa
ya mlipuko ikiwemo kipindupindu kwa kushirikiana na wizara ya
maji,mazingira pamoja na elimu.Vile vile alishauri Serikali kuongeza
nguvu katika huduma ya mama wajawazito pamoja na kuwekeza katika
magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo hivi sasa yanaongezeka kwa kasi na
kuathiri jamii
(Picha na Wizara ya Afya)
|
No comments:
Post a Comment