Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Kazi,
Vijana na Ajira ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini mkoani
Dodoma, Mhe.Antony Peter Mavunde, akizungumza katika ufunguzi wa
Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza.
Kongamano hilo ambalo limeandaliwa kwa
ushirikiano wa pamoja kati ya taasisi ya "Tanzania Youth
Enterpreneurship Organization-TAYEO) pamoja na Vijana Mwanza Saccos,
linafanyika katika viwanja wa Gandh Hall Jijini Mwanza kwa siku mbili,
leo Julai 16,2016 hadi kesho Julai 17,2016 ambapo mgeni Rasmi
anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.
Nape Nhauye.
Wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo
taasisi ya Desk and Chair Foundation, Mfuko wa Hifadhi ya jamii PPF,
Kampuni ya mafuta ya Petro Africa, Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Ofisi
ya mbunge wa jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula, Ofisi ya mbunge wa
jimbo la Ilemela, Mhe.Angelina Mabula ambae pia ni Naibu waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, City Fm na Mhe.Jumanne Kishimba
ambae ni mbunge wa jimbo la Kahama Mjini.
Na BMG
|
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kiburwa Kibamba (kulia), wakifuatilia kongamano hilo. |
Viongozi pamoja na wadau mbalimbali wakiwa katika kongamano hilo. |
Waandaaji wa Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza |
Mwenyekiti wa Shirika la Machinga mkoani Mwanza (katikati) akiwa pamoja na wadau wengine katika Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza. |
Wadau mbalimmbali wakiwa katika Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza. |
Wadau mbalimmbali wakiwa katika Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza.
Vijana mkoani Mwanza wameaswa kutambua
fursa za kiuchumi zilizopo kwenye maeneo yao na kuzitumia kikamilifu ili
kupambana na uhaba wa ajira unaosababisha kukithiri kwa umasikini katika jamii.
Akifungua hii leo kongamano la siku mbili la
vijana kutoka wilaya zote saba za mkoa wa Mwanza, Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde, amesema mkoa wa Mwanza
unazo fursa nyingi za kiuchumi ikiwemo ardhi kwa ajili ya kilimo na Ziwa
Victoria kwa ajili ya uvuvi,hivyo vijana wanapaswa kuzitumia ipasavyo fursa hizo.
Amesema kumejengeka tabia miongoni mwa
vijana kulalamikia uhaba wa ajira jambo ambalo amesema linasababishwa na vijana
hao kushindwa kujitambua huku wengine hasusani wanaohitimu vyuo vikuu wakichagua
kazi za kufanya hivyo kuongeza idadi ya vijana wasio na ajira mitaani.
Aidha Naibu Waziri Mavunde amezitaka
Halmashuri zote nchini kuhakikisha zinatenga asilimia tano ya fedha za mapato
mbalimbali kwa ajili ya kuwawezesha vijana huku pia akiwaagiza wakuu wa
mikoa, wilaya na wakurugenzi wa Halmashuri kutenga maeneo kwa ajili ya vijana na
akina mama kufanya biashara zao bila kubughudhiwa.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa
jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, amesema Halmashauri ya jiji hilo
itahakikisha
inatenga asilimia tano ya mapato yake kwa ajili ya vijana na akina mama
huku akiwataka vijana kuhamasisha wananchi kulipa kodi ili fedha hizo
zipatikane.
Awali akisoma risala kwa niaba ya waandaali wa kongamano hilo, Flora Magabe, amesema
vijana wa mkoa wa Mwanza wamepanga kuwekeza kwenye kilimo na ufugaji wa kuku na
kuiomba serikali kuwapatia maeneo kwa ajili ya kuendesha miradi hiyo.
Kongamano la
Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza, limeandaliwa kwa
ushirikiano wa pamoja kati ya taasisi ya Vijana Wajasiriamali Tanzania
(Tanzania Youth Enterpreneurship Organization-TAYEO) pamoja na Chama cha
Akiba na Mikopo cha Vijana Mwanza Saccos, ambapo linafanyika katika
viwanja wa Gandh Hall Jijini Mwanza, leo na kesho.
|
No comments:
Post a Comment