Katika kuhakikisha kunakuwa na
usalama wa maji duniani kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya vifo
ambavyo vinatokana na uchafu katika maji, Shirika la Umoja wa Mataifa
linalohusika na Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limefanya kongamano
la siku moja ambalo limewakutanisha viongozi wa idara za maji za mikoa
mbalimbali nchini na kutoka nje ya nchi.
Katika kongamano hilo mgeni
rasmi alikuwa ni Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali za Maji kutoka Wizara
ya Maji na Umwagiliaji, George Lugomela alisema sehemu kubwa ya vyanzo
vya maji zimekuwa vikichafuliwa kutokana na usafi wa binadamu.
Alisema kuwa takwimu
zinaonyesha ni asilimia 24 ya watu Afrika ndiyo wanajisaidia katika
maeneo ambayo ni salama na idadi iliyobakia wamekuwa wakijisaidia
mazingira ambayo yanahatarisha vyanzo vya maji na wengi wao wakijisaidia
maporini
|
Mkurugenzi Msaidizi wa
Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji, George Lugomela
akitoa hotuba kwa niaba ya serikali katika kongamano hilo. (Picha na Modewjiblog)
“Kongamano hili linaangalia
kuhusu vijidudu vilivyo katika maji ambavyo kwa asilimia kubwa
yanachafuka kutokana na usafi ambao anaufanya binadamu na ukiangalia kwa
nchi zetu inaonyesha bado uhifadhi wa hizo taka kama kinyesi ambacho
baadae huathiri vyanzo vya maji ni mdogo,” alisema Lugomela.Aidha
alisema pamoja na maeneo mengine kufanya ujenzi wa vyoo lakini jambo
hilo bado sio salama kwa asilimia 100 na hivyo inahitajika kufanyika
jitihada za ziada ili kuweza kuviweka vyanzo vya maji katika hali ya
usalama. |
Mshauri Mwandamizi wa UNESCO, Bruno Nguyen, akielezea umuhimu wa kongamano hilo.
Nae Mshauri Mwandamizi wa UNESCO, Bruno Nguyen, alisema kuwa
kongamano hilo lina malengo ya kupata suluhisho ili kuhakikisha watu
ambao wanaishi bara la Afrika wanapata maji safi na salama. Katika ripoti ya mwaka 2014 ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya (WHO) inaonyesha kuwa watu bilioni 1.8 duniani kote wanatumia maji ambayo yana vijidudu. |
Mtaalam wa programu wa UNESCO, Alexandros Makarigakis akitoa takwamu za usalama wa maji na jinsi taka mwili za binadamu zinavyoyafanya maji yasiwe salama. |
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja. |
No comments:
Post a Comment