Vikosi vya usalama
nchini Uturuki vinasema kuwa zaidi ya maafisa 8,000 wa polisi
wamefutwa kazi, kufuatia jaribio la mapinduzi lililozimwa wiki
iliyopita.
Runinga rasmi ya serikali nchini Uturuki- Anadolu,
inasema kuwa maafisa wengine waliokamatwa ni pamoja na majenerali wakuu
wa kijeshi.
Takriban wanajeshi elfu 6,000 na wahudumu wa mahakama nao pia wamekamatwa.
Vyombo vya habari vinasema kuwa maafisa hao
wanalaumiwa kwa kuwa na uhusiano na mapinduzi hayo ambayo serikali
inadai kuwa yalipangwa na kiongozi wa dini aliyeko uhamishoni nchini
Marekani- Fethullah Gulen.
Msako dhidi ya maafisa wa usalama waliohusika na mipango ya kuipindua serikali juma lililopita nchini Uturuki, unaendelea.
Usiku wa kuamkia leo na mapema Jumatatu alfajiri,
zaidi ya maafisa elfu nane 8,000 wa polisi walikamatwa kushauriwa
kuwasilisha bunduki zao na kusimamishwa kazi.
Kituo cha mafunzo ya wanajeshi wa angani mjini cha Istanbul, kilivamiwa na maafisa hao kukamatwa.
Waendesha
mashtaka wameanza kuwahoji kinara mkuu wa jaribio hilo la mapinduzi
ambaye alikuwa kamanda mkuu wa jeshi la angani Akin Ozturk, ambaye ni
miongoni mwa makamanda wakuu 100 waliokamatwa.
Maafisa wanane wa kijeshi walioingia nchini Ugiriki
kwa kutumia Helikopta, wamefikishwa mahakamani katika mji ulioko mpakani
wa Alexandrou-poli, ili kushtakiwa kwa kuingia nchini humo bila idhini.
Uturuki imeomba Ugiriki kuwarejesha nyumbani ili kushtakiwa, lakini mawakili wao wameomba idhini ya uhamiaji
No comments:
Post a Comment