Wafanyakazi
36 kutoka makampuni mbalimbali nchini Afrika ya Kusini ikiwemo
kampuni ya mawasiliano ya Vodacom wameshiriki mpango wa kupanda
mlima Kilimanjaro kuchangia jamii ujulikanao kama TREK4MANDELA na
fedha zitakazopatikana zitasaidia kuwapatia watoto wa kike elimu ya afya
ya uzazi na taulo za kinga wakati wa hedhi kupitia taasisi ya Imbumba
Foundation ambayo inaendesha mradi wa wasichana
ujulikanao kama Caring4Girls nchini humo.
Mpango
huu wa TREK4MANDELA umekuwa ukienda sambamba na makampuni ya Afrika ya
Kusini kushiriki katika shughuli za kijamii kila mwaka kama sehemu
ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muasisi wa Taifa la Afrika ya
Kusini,Hayati Nelson Mandela na kwa mara ya pili kampuni ya Vodacom
Tanzania imedhamini msafara wa wapanda mlima hao kwa kuwapatia
mawasiliano.
Akiongea
wakati wa kuwakabidhi vifaa vya mawasiliano,Mkuu wa Vodacom kanda ya
Kaskazini, Henry Tsamburakis alisema kampuni ya Vodacom Tanzania
imetoa vifaa vya mawasiliano ili kuwezesha msafara wa wapanda mlima hao
hawapati tatizo la mawasiliano na marafiki,ndugu na familia zao
ikiwemo kutuma picha za matukio wawapo katika safari hiyo ya kupanda
mlimani.
"Vodacom
Tanzania tunajivunia kuweza kuwadhamini watalii na baadhi ya
wafanyakazi wa kampuni yetu kutoka Afrika ya kusini kwa mwaka wa pili
mfululizo kwa kudhamini Mfuko
wa Mandela ambapo kila mwaka watalii hawa huja nchini mwetu mwezi wa
saba kupanda mlima wa Kilimanjaro wakiwa na lengo la kuchangisha pesa
kwa ajili ya kusaidia watoto wa kike" alisema Tzamburakis.
Alisema
Vodacom imetoa vifaa maalumu vya mawasiliano (Routers) sita zikiwa
zimeunganishwa katika mtandao wa kasi wa 4G huku zikiwa zimewekewa
vifurushi vya GB 10 watakazoweza
kutumia kwa muda wote watakapokuwa katika zoezi la kupanda mlima
Kilimanajaro .
Akiongea
kwa niaba ya wenzake kwenye msafara huo,Gerry Elsdon ameshukuru Vodacom
kwa kuwafadhili mawasiliano ambayo yatarahisisha safari yao ya
kupanda Mlima hadi kileleni “Kwa niaba ya wenzangu tunashukuru Vodacom
Tanzani kwa kutupatia mawasiliano ya kuendelea kutuunganisha na wenzetu
popote pale walipo”.Alisema Elsdon.
Kwa
upande wake mratibu wa safari hiyo ,Richard Mabaso ambaye ni
mwanzilishi wa taasisi ya Caring4Girls alisema lengo la safari hiyo ni
kuendelea
kuchangisha fedha kwa ajili ya kununua Taulo za kike kwa watoto wa kike
wasio na uwezo ili kuwasaidia kujihifadhi na kuendelea na shughuli zao
za kila siku kama kawaida wakiwa salama na wakijiamini.
"Tunatambua
changamoto zinazowakabili watoto wa kike hasa wale walioko mashuleni
pindi wanapoingia katika siku zao,kupitia Mfuko wa Mandela tumeendelea
kuchangisha pesa kwa ajili ya kuwasaidia angalau kupata taulo ili
waweze kuendelea na masomo bila ya kuwa na kikwazo." alisema Mabaso.
Jitihada
za kupambana na changamoto za vipindi vya hedhi pia zimekuwa zikifanywa
na taasisi mbalimbali hapa nchini mojawapo ikiwa Vodacom Tanzania
Foundation ambayo imekuwa ikifadhili mradi wa Girl Power unaoendeshwa
na Shirika lisilo la kiserikali la T-MARC ambao umewezesha kupunguza
utoro kwa wasichana waliokuwa wanakosa masomo kutokana na kukosa vifaa
vya kuwakinga wakati wa hedhi na kutokuwepo
na miundombinu rafiki mashuleni.
|
No comments:
Post a Comment