Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia
mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma mapema leo asubuhi waliojitokeza
kushuhudia maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa iliyofanyika
kwenye uwanja wa Mashujaa, mjini Dodoma.PICHA NA MICHUZI JR-DODOMA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasihi
watanzania kuwaenzi Mashujaa kwa kudumisha Amani, Umoja na Utulivu
uliojengwa na mashujaa hao.Rais Magufuli ametoa rai hiyo leo tarehe 25
Julai, 2016 wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya Mashujaa,
yaliyofanyika katika uwanja wa Mashujaa Mjini Dodoma.
Pamoja
na kutoa rai hiyo Rais Magufuli ameahidi kuwa atahakikisha azma ya
Serikali kuhamia Dodoma inatekelezwa kabla ya kuisha kwa kipindi chake
cha uongozi wa miaka mitano.
"Tunapoadhimisha
siku ya Mashujaa hatuwezi kumsahau Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa alisema makao makuu yawe Dodoma,
haiwezekani sisi watoto wake, sisi wajukuu wake tupinge kauli ya Mzee
huyu.
"Kwa
hiyo nilikwishazungumza na leo narudia hili katika siku ya Mashujaa,
mlinichagua ndugu zangu wa Dodoma kwa kipindi cha miaka mitano, hadi
sasa miezi minane imepita, nimebakiza miaka minne na miezi minne, nataka
kuwathibitishia kuwa katika kipindi cha miaka minne na miezi minne
iliyobaki nitahakikisha serikali yangu pamoja na mimi tunahamia Dodoma
bila kukosa"Amesema Rais Magufuli.
Kufuatia
maelekezo hayo ya Mhe. Rais, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameagiza Mawaziri wote waanze mara moja
kuhamia Dodoma na kwamba yeye mwenyewe atakuwa amehamia Dodoma ifikapo
mwezi Septemba mwaka huu.
Viongozi
wengine waliohudhuria maadhimisho hayo ni Makamu wa Rais Mhe. Samia
Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan
Mwinyi, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Naibu Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, Spika wa Baraza la
Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid, Mawaziri Wakuu wastaafu Mhe. John
Samwel Malecela na Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda, Mabalozi na
wanadiplomasia kutoka nchi mbalimbali, Viongozi wa vyombo vya ulinzi na
usalama, Viongozi wa vyama vya siasa na dini, maafisa na askari
waliopigana vita mbalimbali.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
25 Julai, 2016
No comments:
Post a Comment