Kiongozi
Mkuu wa ACT, Zitto Kabwe tayari ameondoka nchini kuelekea nchini
Marekani ambao alialikwa na mgombea urais wa nchi hiyo, Hillary Clinton
kuhudhuria mkutano mkuu wa chama cha Democratic.
Akiwa
katika mkutano huo, Zitto anataraji kukutana na kufanya mazungumzo na
viongozi mbalimbali wa kisiasa kutoka mataifa mbalimbali duniani kuhusu
hali za kiasi katika mataifa yao.
Pia
akiwa nchini Marekani anataraji kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa
CUF, Maalim Seif Shariff Hamad kuhusu hali ya kisiasa visiwani Zanzibar
na Tanzania kwa ujumla lakini pia kuanza kufanya maandalizi ya ufunguzi
wa tawi la wanachama wa ACT Diaspora.
Nafasi
abayo ameipata Zitto inaonekana kuwa fursa ya kipekee katika maisha
yake ya kisiasa kwani mkutano atakaohudhuria ndiyo utakaomthibitisha
Hillary Clinton kuwa mgombe urais kupitia chama cha Democratic.
No comments:
Post a Comment