akonta Kapunda : Msichana mwenye umri wa miaka (22) akitumia ulimi kuandika meseji kwenye simu yake ya Mkononi wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Dada yake Bi. Judith Assenga.Binti huyo ameanza kutumia kiungo hicho katika kuandika baada ya kupooza sehemu ya mwili wake kutokana na ajali mbaya aliyoipata mwaka 2012 akiwa na wenzake tisa wakati wa Mahafali ya Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe Mkoani Tanga. |
Msichana mwenye umri wa miaka (22) Bi. Wakonta Kapunda akifanya mahojiano maalum na mwandishi wa Radio ya Kimataifa ya Ufaransa (Rfi) wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Binti huyo anatumia ulimi na simu aina ya Smart Phone katika kuandika baada ya kupooza sehemu ya mwili wake kutoka na ajali mbaya aliyoipata mwaka 2012 akiwa na wenzake tisa Korogwe Mkoani Tanga. |
Kutoka kulia ni Wakonta Kapunda, Judith Assenga(dada yake na Wakonta), Mwajuma Selkemani na Chritina Rubangula(waliokuwa wanafunzi wenzake na Wakonta) wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Wakonta anatumia ulimi na simu aina ya Smart Phone katika kuandika baada ya kupooza sehemu ya mwili wake kutoka na ajali mbaya aliyoipata mwaka 2012 akiwa na wenzake tisa Korogwe Mkoani Tanga |
Baba mzazi wa Wakonta (hayupo pichani) Bw. Brazilio Kapunda akifanya mahojiano maalum na mwandishi wa Radio ya Kimataifa ya Ufaransa (Rfi) wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.Mwenye brauzi nyekundu ni Mama wa binti huyo Bibi. Rahel Lymo,Wakonta anatumia ulimi na simu aina ya Smart Phone katika kuandika baada ya kupooza sehemu ya mwili wake kutoka na ajali mbaya aliyoipata mwaka 2012 akiwa na wenzake tisa Korogwe Mkoani |
Waandishi wa habari wakiwa wameshika karatasi lenye namba ambazo wadau wanaweza kutumia kumchangia Wakonta Kapunda (aliyekaa kwenye kiti cha matairi) ili apatae matibabu na hatimaye kutimiza ndoto zake za kwasaidia wengine wenye matatizo kama yake leo jijini Dar es Salaam.Binti huyo amekusudia kutumia kalama ya uandishi wa Filamu na kuanzisha Taasisi itakayo kuwa msaada kwa watu wenye matatizo ya kupooza. |
Wakonta
Kapunda akiwa katika picha ya pamoja na wazazi wake,Dada yake,
marafaiki zake aliosoma nao shule ya Sekondari Korogwe na mshiriki
mwenzake katika Shindano la uandishi wa Miswada lililofanyika mjini
Zanzibar leo Jijini Dar es Salaam.
Picha Zote na: Frank Shija, MAELEZO.
……………………………………………………………………………………………..
Na: Frank Shija, MAELEZO
Msichana
anayetumia Ulimi katika kuandika miswada ya Filamu amewashukuru wadau
mbambali kwa misaada yao iliyomfanikisha kuweza kushiriki katika
mashindano ya uandishi wa miswada ya Filamu yaliyofanyika mjini
Zanzibar.
Shukuruani
hizo amezitoa leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa anaongea na waandishi
wa habari kuhusu malengo yake ya kuanzisha Taasisi itakayosaidia watu
wenye matatizo kama yake.
Wakonta
amesema kuwa kwa namna ya kipekee kabisa anaishukuru Serikali ya Awamu
ya Tano kupitia kwa Bodi ya Filamu kumgharamia nauli iliyomsaidia kutoka
kijijini kwa Kipili wilayani Nkasi mkaani Rukwa hadi kuanikisha
ushiriki wake katika mashindano hayo.
“Ninaishukuru
sana kwa kipekeke Serikali ya awamu ya Tano, kwani kupitia kwa KatIBU
Mtendaji wa Bodi ya Filamu nimeweza kusaidiwa fedha iliyoniwezesha
kushiriki katika mashindano ya Uandishi wa Miswada ya Filamu nashukuru
sana”. Alisema Wakonta.
Aliongeza
kuwa pamoja na Serikali kumpa msaada huo wapo baadhi ya wadau ambao nao
wametoa michango yao katika kufanikisha Kampeni yake ambapo amewataja
wadau hao kuwa ni Clouds Media waliomsaidia kuhabarisha umma, Joyce
Kiria aliye safiri hadi kijijini kwao Kipili ili kumsaidia kupitia
kipindi chake cha Wanawake Live.
Wengine
ni pamoja na magazeti ya Mwananchi na Uwazi kupitia waliokuwa msaada
kupitia habari zao, Fastjet waliomsaidia huduma ya usafiri kutoka Mbeya
na Hoteli ya Serena waliomsaidia upande wa malazi wakati alipofika Dar
es Salaam akitoea kijini kwao Kipili, Mkoani Rukwa.
Ametoa
rai kwa wadau wenye nafasi zao kujitokeza na kushirikina naye katika
kukuza kipaji chake ili aweze kukitumia katika kuleta tija kwa Taifa
kwani kupitia Filamu unaweza kutangaza Utalii wanchi na ata biashara.
Wakonta alikuwa miongoni mwa washiriki 15 kutoka Afrika Mashariki katika Shindano la Uandishi wa Miswada ya Filamu la Maisha Scree Writer’s Laboratory Course lililofanyika mjini Zanzibar na huku yeye akiwa mshiriki pekee anayetumia Ulimi katika kuandika.
|
No comments:
Post a Comment