Mkutano Mkuu wa viongozi wa Afrika jijini Kigali nchini Rwanda
Viongozi
wa mataifa ya Afrika wameshindwa kumchagua Mwenyekiti mpya wa Tume ya
Umoja huo katika mkutano ya viongozi hao jijini Kigali nchini Rwanda.
Hii
inamaana kuwa Mwenyekiti wa sasa Nkosazana Dlamini-Zuma ambaye alikuwa
ametangaza kutowania tena wadhifa huo ataendelea kuongoza hadi mwezi
Januari mwaka ujao wakati uchaguzi mwingine utakapofanyika.
Msemaji
wa Dlamini Zuma, Jacob Enoh Eben kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema
baada ya mzunguko wa kwanza wa upigaji kura na kubainika kuwa hakuna
mgombea aliyepata theluthi mbili ya kura ili kupata mshindi huku mataifa
28 kati ya 54 yakisusia zoezi hilo la kupiga kura.
Kulikuwa
na wagombea watatu, aliyekuwa Makamu wa rais wa Uganda Specioza Wandira
Kazibwe, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya nje wa Bostwana Pelonomi
Venson-Moitoi na Agapito Mba Mokuy ambaye pia alikuwa Waziri wa zamani
wa Mambo ya nje ya Equatorial Guinea.
Wiki
iliyopita, kulikuwa na wasiwasi ikiwa uchaguzi huu ungekuwepo wakati wa
kikao hiki cha 27 kwa madai kuwa hapakuwa na mgombea sahihi wa kuchukua
nafasi ya Bi.Zuma kutokana na ushawishi wa mataifa yenye uchumi mkubwa
barani Afrika kama Nigeria na Afrika Kusini.
Majukumu
makubwa ya Mwenyekiti mpya itakuwa ni kushughulikia maswala ya amani,
usalama na siasa barani Afrika, biashara na viwanda, miundo mbinu,
maswala ya kijamii na Sayansi na teknolojia.
Dlamini Zuma kutoka Afrika Kusini alichaguliwa katika nafasi hiyo mwaka 2012 na kuchukua nafasi ya Jean Ping kutoka Gabon |
July 19, 2016
VIONGOZI WA AFRIKA WASHINDWA KUMCHAGUA MWENYEKITI MPYA WA TUME YA AU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment